Yanga yatanguliza mguu mmoja makundi Afrika
DAR ES SALAAM; Yanga ya Dar es Salaa imetanguliza mguu mmoja hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya leo kuibuka na ushindi wa mabao 0-4 dhidi ya CFFA ya Madagascar kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam. Timu hiyo ya Madagascar imetumia Uwanja wa Azam Complex kama uwanja wa nyumbani na zitarudiana …
DAR ES SALAAM; Yanga ya Dar es Salaa imetanguliza mguu mmoja hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya leo kuibuka na ushindi wa mabao 0-4 dhidi ya CFFA ya Madagascar kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Timu hiyo ya Madagascar imetumia Uwanja wa Azam Complex kama uwanja wa nyumbani na zitarudiana baada ya wiki moja, ambapo Yanga itakuwa mwenyeji kwenye uwanja huohuo, ikihitaji ushindi wowote, au hata sare ya aina yoyote au isifungwe zaidi ya mabao 3 itakuwa imesonga mbele na kutinga makundi.
Yanga imetinga hatua hiyo baada ya kuitoa Gaborone United ya Botswana kwa jumla ha mabao 3-2, ambapo mchezo wa kwanza Botswana zilitoka sare ya bao 1-1 na ziliporudiana Dar es Salaam, Yanga ilishinda mabao 2-1.
CFFA iliingia hatua hiyo baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Lijabatho ya Lesotho kwenye mchezo wa awali kabla ya kushinda mabao 2-0 mchezo wa marudiano.