Wawili waachiwa kesi uhujumu bil 5.7/-

Habari Leo
Published: Jan 26, 2026 08:49:26 EAT   |  News

MKURUGENZI wa Mashitaka (DPP) amesema hana nia ya kuendelea kuwashitaki washitakiwa wawili kati ya 10 wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ya kuongoza genge la uhalifu na kujipatia zaidi ha Sh bilioni 5.7 kwa njia za udanganyifu.

The post Wawili waachiwa kesi uhujumu bil 5.7/- first appeared on HabariLeo.

MKURUGENZI wa Mashitaka (DPP) amesema hana nia ya kuendelea kuwashitaki washitakiwa wawili kati ya 10 wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ya kuongoza genge la uhalifu na kujipatia zaidi ha Sh bilioni 5.7 kwa njia za udanganyifu.

Washitakiwa hao ni aliyekuwa mshitakiwa namba tatu, Caroline Masanyika na namba 10, Claude Beda. Washitakiwa waliobaki ni mfanyabiashara, Fredrick Elphas Ogenga, Ofisa wa benki benki ya Equity makao makuu, Lilian Koka, Halifa Maina, Kaizilege Mohamed, Daudi Fata, Mrisho Mrisho, Neema Paul na Jefferson Ogenga.

Wakili Mkuu wa Serikali, Caren Mrango akisaidiana na Wakili wa Serikali, Titus Aaron alieleza hayo wiki iliyopita katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franco Kiswaga kesi hiyo ilipotajwa. Wakili Caren alidai shauri hilo lilipelekwa kwa ajili ha kutajwa lakini aliomba kuiarifu mahakama DPP hana nia ya kumshtaki mshtakiwa Caroline na Beda.

Amesema washitakiwa hao waondolewe chini ya kifungu 92 (1) cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) Sura ya 20 marejeo 2023. Pia, aliomba kuieleza mahakama hiyo kuwa wapo katika hatua za mwisho za upelelezi wa jalada hilo na muda wowote kuanzia siku hiyo wanaweza kusajili taarifa katika mahakama yenye mamlaka.

Wakili wa Utetezi, Steven Moshi amedai kuwa  vikao vya makubaliano ya kukiri kosa na DPP kwani washitakiwa waliomba vikao hivyo vitolewe taarifa namna vinavyoendelea kwa sababu mawakili wa serikali hawasemi wamefikia wapi.

Hakimu Kiswaga aliahirisha shauri hilo hadi Februari 4, 2026 itakaposikilizwa kwa njia ya mtandao. Washitakiwa waliobaki walirudishwa rumande. Kwa mujibu wa hati ya mashitaka washtakiwa wanadaiwa kati ya Agosti 30, 2024 hadi Juni 28, 2025 katika maeneo tofauti ndani ya Dar es Salaam waliongoza genge la uharifu na kujipatia Sh bilioni 5.7 mali ya Benki ya Equity Tanzania Limited.

Ilidaiwa katika tarehe hizo mshitakiwa Jasmine na Ogenga wakiwa ndani ya makao makuu ya Benki ya Equity iliyopo Ilala, waliiba Sh bilioni 3.6 zilizokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika akaunti ya clearing and settlement, mali ya Benki ya Equity. SOMA: Raia wa India kortini kesi ya uhujumu uchumi

Mshitakiwa Caroline katika tarehe hizo, akiwa katika Makao Makuu ya Benki ya Equity iliyopo Ilala, anadaiwa kuiba Sh milioni 728, mali ya benki hiyo. Pia, ilidaiwa kati ya Februari 28 na Aprili 2, 2025 makao makuu ya benki hiyo, Lilian aliiba Sh milioni 26 kutoka akaunti ya benki hiyo.

Pia, kati ya Januari Mosi hadi Aprili 24, 2025 katika benki hiyo, Maina aliiba Sh milioni 101, mali ya benki hiyo. Ilidaiwa, kati ya Januari 22 hadi Aprili 24, 2025 katika ofisi hizo za benki hiyo, Mohamed aliiba Sh milioni 57 huku Fata akidaiwa kuiba Sh milioni 758, tukio analodaiwa kulitenda kati ya Novemba 2, 2024 hadi Mei 25, 2025.

The post Wawili waachiwa kesi uhujumu bil 5.7/- first appeared on HabariLeo.