Wasomi wa Kiswahili wamuomboleza Profesa Hamu Habwe

Taifa Leo
Published: Aug 18, 2025 10:03:51 EAT   |  Educational

WAPENZI wa Kiswahili nchini na kanda nzima ya Afrika Mashariki wanaomboleza kifo cha msomi na mwandishi Profesa John Hamu Habwe ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 62. Profesa Habwe alifariki akitibiwa hapo Jumapili katika hospitali moja jijini Nairobi baada ya kuugua kwa zaidi ya miaka mitatu. Alizaliwa na Mzee Hamu Jonah na mama Alice Apasi Hamu ameacha mjane Teresa Habwe na watoto. Profesa Habwe ambaye alizaliwa katika Kijiji cha Ebukhaya, Emabuye kaunti ndogo ya Emuhaya mnamo mwaka wa 1963 ni Profesa wa kwanza katika kata ya Ebukhaya. Kwa muujibu wa kakake mdogo Astaricus Hamu ni kwamba marehemu alikuwa nguzo muhimu katika familia yao. “Profesa alikuwa nguzo muhimu katika jamii yetu hatujawahikuwa na mtu msomi mwenye kujali watu wake kama ndugu yangu. Mungu ailaze roho yake pema peponi.” alisema. Profesa Habwe alianzia masomo yake katika shule ya msingi ya Ebukhaya katika ilokuwa kata ya North Bunyore miaka ya sabini kabla ya kujiunga na shule ya upili ya Ebwali East Bunyore miaka ya themanini na hatimaye kujiunga na shule ya upili ya Kapkatet Boys kaunti ya Kericho kwa kidato cha sita. Mwishoni mwa miaka ya themanini. Alijiunga na chou kikuu cha Nairobi idara ya Lugha ya Kiswahili mapema miaka ya tisini kabla ya kufundisha katika shule mbalimbali eneo la Bunyore na hatimaye kuwa mkufunzi katika chuo kikuu cha Nairobi. Amefundisha katika chuo hicho kwa zaidi ya miaka 30 hadi mwaka wa 2016. Alipokuwa katika chuo kikuu cha Nairobi alipata kuhudumu kama mwenyekiti wa idara ya Kiswahili na lugha nyingine za kiafrika kwa miaka miwili . Mbali na kuwa mwalimu ameandika vitabu kadha na kushiriki warsha za Kiswahili na kutoa shauri kwa wataalam wa lugha ya Kiswahili kupitia kwa vipindi vya redio na runinga haswa KBC. Marehemu aliwahifundisha katika vyuo vingine ikiwa ni Pamoja vyuo vikuu vya Moi, Maseno na chuo kikuu cha Catholic University. Vile vile amefanyakazi katika mashirika ya kimataifa kama vile shirika la chakula na na killimo FAO, World Health Organization (WHO)  na tume ya Afrika Mashariki yani Kiswahili Commission of East Africa kama mtafsiri. Ameandika vitabu vya watoto miongoni mwa vitabu vingine ikiwa ni Pamoja na kitabu chake cha Kwanza ‘Maumbile si huja’. Mipango ya mazishi inaendelea,marehemu atazikwa katika shamba lake Lugari katika kaunti ya Kakamega.