WANTAM: Seneta amshinda Rais wa Brazil katika duru ya kwanza ya uchaguzi, waelekea duru ya 2
SENETA Flavio Bolsonaro amefuzu kwa raundi ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Brazil baada ya kumpiku kwa tofauti ndogo Rais wa sasa Luiz Inacio Lula da Silva katika uchaguzi mkuu.
Bolsonaro, mwanawe rais wa zamani, Jair Bolsonaro, alipata asilimia 47 ya kura dhidi ya asilimia 45 za Lula.
Matokeo hayo yalikuwa kinyume na utabiri wa kura za maoni, ambazo zilitarajia Lula kuongoza kwa tofauti ya karibu asilimia tatu.
Sasa wawili hao watamenyana katika uchaguzi wa mwisho utakaofanyika Oktoba 25.
Baada ya matokeo, Flavio alisema raia wa Brazil wanataka mabadiliko na kutangaza kile alichokiita mwisho wa enzi ya chama cha Lula cha Workers’ Party.
Lula, ambaye alitarajia kushinda katika raundi ya kwanza, aliwaambia wafuasi wake kuwa kampeni mpya inaanza mara moja na akaahidi kuwaeleza wapigakura mafanikio ya serikali yake.
Uchaguzi huo ulitawaliwa zaidi na masuala ya gharama ya maisha, ukosefu wa usalama na ufisadi.
Licha ya kupungua kwa tatizo la uhaba wa ajira na tofauti za kimapato, Lula amekabiliwa na changamoto ya kuwashawishi wananchi wanaolalamikia gharama kubwa za maisha, madeni ya kifamilia na ongezeko la shughuli za magenge.
Flavio ametumia hali hiyo kuomba kura za mabadiliko, huku Lula akipanua mipango ya ustawi wa jamii na kupendekeza msamaha wa baadhi ya madeni ya familia.
Uchumi pia ulikuwa suala muhimu, huku matumizi ya serikali yakiongezeka na deni la umma kufikia zaidi ya asilimia 82 ya pato la taifa. Serikali pia ilipunguza utabiri wa ukuaji wa uchumi wa Brazil mwaka huu hadi asilimia mbili.
Uchaguzi huo pia ulikumbwa na mijadala kuhusu ufisadi na madai ya kuingiliwa kutoka nje.
Jair Bolsonaro, baba yake Flavio, anatumikia kifungo cha miaka 27 kwa kupanga mapinduzi baada ya kushindwa uchaguzi wa 2022.
Flavio sasa anajaribu kutumia urithi wa kisiasa wa baba yake kumpinga Lula.
Ingawa Rais wa Amerika, Donald Trump hajamtangaza rasmi mgombeaji anayemuunga mkono, amekuwa akimsifu Flavio na kumkaribisha Ikulu ya White House.
Kwenye raundi ya pili, Brazil sasa inakabiliwa na ushindani mkali kati ya mrengo wa kushoto unaoongozwa na Lula na mrengo wa kulia unaowakilishwa na Bolsonaro.
Matokeo hayo pia yanaonyesha mgawanyiko mkubwa wa kisiasa nchini Brazil, huku Flavio akifanya vizuri zaidi katika maeneo ya Kusini, Kusini-Mashariki na Kati-Magharibi, wakati Lula aliongoza katika ngome zake za Kaskazini-Mashariki pamoja na baadhi ya majimbo ya Kaskazini.
Kwa upande mwingine, wapigakura waliowaunga mkono wagombeaji wengine sasa wanakuwa muhimu katika raundi ya pili.
Augusto Cury alipata karibu asilimia 2.9, Renan Santos asilimia 2.2 na Ronaldo Caiado asilimia 2.2, huku wagombeaji wengine wakigawana sehemu ndogo ya kura.
Ushiriki wa wapigakura pia ulikuwa suala muhimu, kwani takriban asilimia 21 ya wapigakura waliojiandikisha hawakupiga kura.
Asilimia 2.93 ya kura ziliharibika na asilimia 1.84 zikawa “nyeupe” (mpigakura kutochagua mwaniaji yeyote), hali inayomaanisha kuwa sehemu kubwa ya wapigakura ambao hawakuwachagua wagombea hao wawili bado inaweza kuwa muhimu katika raundi ya mwisho.
Kwa Flavio, ushindi huo wa raundi ya kwanza umempa nafasi ya kuendeleza urithi wa kisiasa wa familia ya Bolsonaro, huku Lula akilenga kuunganisha wafuasi wake na kupata kura za wagombea walioshindwa.
Kwa kuwa tofauti kati yao ilikuwa chini ya asilimia mbili, kampeni ya kuelekea Oktoba 25 inatarajiwa kulenga zaidi masuala ya uchumi, usalama, ustawi wa jamii na mwelekeo wa kisiasa wa Brazil.