Wanawake wanufaikia zabuni za serikali kwa asilimia 58

Taifa Leo
Published: May 05, 2026 09:03:57 EAT   |  General

BIASHARA za wanawake ndizo zimekuwa  zikinufaikia nafasi za utoaji zabuni za serikali, hii ni kwa mujibu wa takwimu kutoka Mamlaka ya Kudhibiti Utoaji Zabuni katika Sekta ya Umma ((PPRA).  Kinaya ni kwamba kunufaika huku hakujakuwa na tija sana kwa sababu biashara hizi zinakosa mabilioni ya pesa kutokana na vikwazo vya kiuchumi. Takwimu kutoka PPRA na Hazina Kuu ya Kifedha zinaonyesha kuwa biashara za wanawake zilipata kandarasi ambazo ni thamani ya Sh33.1 bilioni mwaka wa kifedha ambao ulikamilika mnamo Juni 2025. Hii inawakilisha asilimia 58.3 ya Sh56.8 bilioni ambazo zilitolewa chini ya mpango wa serikali wa utoaji zabuni maarufu kama AGPO. Hii inaonyesha kuwa makundi ya wanawake ndiyo yalinufaika zaidi na zabuni hiyo. Hata hivyo, Shirika la Women Kenya nalo limesema takwimu hizo zinastahili kuwa zimepanda zaidi kwa sababu wanawake wanapokea asilimia 18.1 pekee ya nafasi za mipango ya AGPO. Hii ni chini ya asilimia 30 ambazo wanawake wametengewa  chini ya Sheria za Utoaji Zabuni kwa Umma mnamo 2015. Mwenyekiti wa Taasisi ya Udhibiti na Usambazaji Bidhaa (KIMS) Jennifer Cirindi Njiru aliwataka alisikitika kuwa japo wanawake ni zaidi ya nusu wanaofaka kazi kwenye sekta ya utoaji zabuni, chini ya asilimia 20 wanashikilia vyeo vya ngazi ya juu. Bi Njiru aliwataka washikadau wasishiriki mazungumzo tu bali pia wanawake washirikishwe katika utekelezaji wa sera kwenye sekta ya utoaji zabuni. Alikuwa akiongea kwenye kongamano lililoandaliwa Mombasa na kuhusisha washikadau na wafanyakazi kwenye sekta ya utoaji wa zabuni. Kutakuwa na Kongamano jingine la kiuchumi la wanawake maarufu kama SHEconomy kati ya Mei 28-29 Nairobi ambalo litahudhuriwa na zaidi ya wanawake 1,000 wafanyabiashara, wanakandarasi na wafanyabiashara ndogondogo kutoka kaunti zote 47. Mwanzilishi wa Kampuni ya Recolte Betty Karimi ndiyo atakuwa mwenyeji wa kongamano hilo litakaloangazia nafasi za tenda kwa wanawake na masuala yanayohusu kandarasi za kibiashara. “Tupo katika wakati ambapo masuala ya uchumi sasa yanachukua mkondo mpya. Sisi ndio nguzo wa uchumi na wanawake ndio wataleta mageuzi haya,” akasema Bi Karimi.  