Wanahabari wa Nation Media wavamiwa na kuporwa Thika Road
WANAHABARI wa Nation Media Group (NMG) ambao walikuwa wakifuatilia maandamano ya bei za juu ya mafuta katika barabara ya Thika, jana walivamiwa na kuibiwa na wahuni.
Gari ambalo lilikuwa na wanahabari hao lilizingirwa na wahuni hao kisha wakaporwa. Wavamizi hao waliziba barabara kwa mawe na kuitisha hela kabla gari halijapita.
Waliovamiwa walikuwa wanabari wa runinga ya NTV na Daily Nation ambao walikuwa wakirejea Nation Center baada ya kufuatilia maandamano na mgomo wa wahudumu wa matatu miji ya Ruiru na Juja.
Walivamiwa katika eneo la Ruiru Bypass.
Genge hilo liliingia barabarani, likazunguka gari lao na kuwarushia mawe. Walichukua fulani mbili za kuwatambua kama wanahabari, helmeti kisha kuwapora kamera na mkoba wa kubeba kamera hiyo.
Waliokuwa kwenye gari hilo ni ripoti wa runinga ya NTV Labaan Shabaan, mnasa video wa NTV Luis Ngari, ripota wa Daily Nation Kevin Cheruiyot, mpiga picha Evans Habil na dereva wao Bernard Magara.
Walipiga ripoti kuhusu uporaji huo katika kituo cha polisi cha Gatongora na bado hali ilikuwa tete eneo hilo waandamanaji wakiziba barabara.