Wanafunzi vyuo vikuu washauriwa lishe bora
MOROGORO: MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Morogoro, Lucy Kombani amewashauri wanafunzi wa vyuo vikuu kuzingatia ulaji wa vyakula vyenye lishe bora kwa ajili ya kujenga afya zao ili waepukane kupatwa na maradhi yanayosababishwa na lishe duni . Kombani amesema hayo kwenye mada yake wakati wa kongamano la University ladies and Gentleman 2026 lililoandaliwa na …
The post Wanafunzi vyuo vikuu washauriwa lishe bora first appeared on HabariLeo.
MOROGORO: MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Morogoro, Lucy Kombani amewashauri wanafunzi wa vyuo vikuu kuzingatia ulaji wa vyakula vyenye lishe bora kwa ajili ya kujenga afya zao ili waepukane kupatwa na maradhi yanayosababishwa na lishe duni .
Kombani amesema hayo kwenye mada yake wakati wa kongamano la University ladies and Gentleman 2026 lililoandaliwa na Taasisi ya Ladies Talk Tanzania katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Jordan, mjini Morogoro.
Kongamano hilo lilifunguliwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara , Dennis Londo na kushirikisha wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA),Chuo Kikuu Mzumbe na Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro.
Wengine ni Chuo Kikuu Kishiriki cha Jordan ,Chuo cha Ualimu Morogoro, Chuo cha St Joseph, Chuo cha Mifugo (LITA), Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro (MSJ),na wanafunzi wa shule za Sekondari Morogoro na Mafiga.
Mbunge huyo ameshauri wanafunzi wa vyuo vikuu kujenga tabia ya kupangilia vizuri milo yao yenye kuzingatia makundi yote muhimu yenye virutubishi vya lishe bora kwa ajili ya kujenga afya zao .
“ Wanafunzi kuleni vizuri, mnaingia vyuo unapata Boom ( fedha ya kujimu, kwa ajili ya chakula na matumizi mengine madogo madogo ya mwanafunzi) kwa maana mwezi mzima wanafunzi anapanga kula chips mayai na soda , kesho yako inaangalia pia na afya yako , unavyokula leo ndiyo kesho yako inavyokuwa, hivy o kuweni makini na aina ya chakula unachokula “ amesisitiza Kombani.
Kombani pia amewasihi wanafunzi wanapokuwa vyuoni wejenge tabia ya kumcha Mungu kwani imebainika baadhi ya wanafunzi wanapofika vyuoni yanabadirika tabia zao na kuacha kwenda kumwabudu Mungu.
Mbunge huyo pia amesema vijana ni rasilimali watu muhimu ya sasa na baadaye katika Taifa letu , hivyo kusoma kwao katika vyuo mbalimbali ni njia ya kuwaanadaa ili walitumikie vyema nchi yao.
“Kama mada kuu inavyosema tumia elimu yao kujenga kesho yako,” amesema Mbunge Kombani.
Mbunge Kombani amewashauri vijana wa vyuo vikuu kujenga misingi ya kujitengemea wakitambua ni muda muafaka wa kujifunza kujenga kesho yao ili kufikia malengo yao kwa njia ya kujitegemea.
Kombani amesema Serikali imesisitiza umuhimu wa mafunzo ya ufundi stadi ,biashara na ujasiriamali, na hivyo kuwataka vijana kutumia mitandao ya kijamii kujufunza masuala hayo ya ufundi stadi.
Kwa upande wake Ofisa Maadili Mwandamizi, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ,Kanda ya Mashariki, Zaynab Kissoky katika mada yake amesema maadili ni msingi wa kudumu katika kufikia malengo mazuri ya nyanja mbalimbali .
Zaynab amesema maadili ni kufanya kitu kilicho sahihi wakati wote na kwamba vijana wanapofanya maamuzi yasiyo sahihi nyakati wakiwa vyuoni inawatanya kwenda kuvunja maisha ya kesho yao.
“Maadili ni mtaji, maadili ni kuwa na nidhamu binafsi, uaminifu, heshima, uwajibikaji na tabia nzuri itakufikisha mbali kuliko akili peke yake na akili peke yake haiwezi kukufungulia milango,” amesema Zaynab.
The post Wanafunzi vyuo vikuu washauriwa lishe bora first appeared on HabariLeo.