Wakenya wafurika kuuaga mwili wa Odinga

KENYA: Maelfu ya wananchi wa Kenya wamejitokeza katika Uwanja wa Jomo Kenyatta, Mamboleo ulioko, Kaunti ya Kisumu, Kenya kuaga mwili wa Hayati Raila Odinga leo Oktoba 18, 2025. Raila Odinga alifariki dunia Oktoba 15, nchini India ambako alikuwa akipatiwa matibabu. Baadhi ya wananchi waliozungumza na HabariLeo wamesema Odinga atakumbukwa kwa kuwaunganisha Wakenya bila kujali tofauti …
The post Wakenya wafurika kuuaga mwili wa Odinga first appeared on HabariLeo.
KENYA: Maelfu ya wananchi wa Kenya wamejitokeza katika Uwanja wa Jomo Kenyatta, Mamboleo ulioko, Kaunti ya Kisumu, Kenya kuaga mwili wa Hayati Raila Odinga leo Oktoba 18, 2025.
Raila Odinga alifariki dunia Oktoba 15, nchini India ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na HabariLeo wamesema Odinga atakumbukwa kwa kuwaunganisha Wakenya bila kujali tofauti zao.
Wametaja baadhi ya mambo hayo kuwa ni kupigania usawa na haki za binadamu na utawala bora.
Mwili wa Odinga utazikwa kesho Oktoba 20, 2025, katika shamba lake la Opoda, Kaunti ya Siaya.
The post Wakenya wafurika kuuaga mwili wa Odinga first appeared on HabariLeo.