Wageni watajwa ongezeko la VVU Manispaa Moro, Ifakara
MOROGORO; Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro, Dk Mussa Ali Mussa amesema ongezeko la maambukizi mapya ya VVU Manispaa ya Morogoro na halmashauri ya Mji Ifakara kunatokana na kuwepo kwa wageni wengi. Dk Mussa amesema hayo mbele ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya Ukimwi, Dk Zeyana Abdallah Hamid, …
MOROGORO; Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro, Dk Mussa Ali Mussa amesema ongezeko la maambukizi mapya ya VVU Manispaa ya Morogoro na halmashauri ya Mji Ifakara kunatokana na kuwepo kwa wageni wengi.
Dk Mussa amesema hayo mbele ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya Ukimwi, Dk Zeyana Abdallah Hamid, ilipofanya ziara mkoani Morogoro na kutembelea Kituo cha Afya Kingolwira , Manispaa ya Morogoro pamoja na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) .
Amesema kuongezeka kwa maambukizi mpaya kwa Manispaa ya Morogoro kunachangiwa na ujio wa wageni wengi pamoja uwepo wa vyuo vingi vyenye kukusanya vijana wengi, jambo ambalo linaweza kuchangia ongezeko la mambukizi mapya ya VVU.
Kwa upande wa Mji Ifakara Dk Mussa ameeleza wenyewe ni m ji wa kibiashara ambaao pia unajumisha makabila mengi na wengi wao wanavutiwa na shughuli za kilimo , biashara pamoja na kuwepo wafugaji wenye wenye kuhamahama.
Dk Mussa amesema kwa sasa juhudi zinaendelea kuchukuliwa, zikiwa na utoaji wa elimu kwa makundi mbalimbali ya kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi mapya.
Naye Mratibu wa Ukimwi na Magonjwa ya Ngono na Homa ya Ini Mkoa wa Morogoro , Dk Shigela Marco, amesema utafiti wa Tanzania HIV impact Survey (THIS) wa Mwaka 2022/2023 ulionesha maambukizi ya VVU kwa mkoa huo ni asilimia 3.3 , wanawake asilimia 3.6 na wanaume asilimia 2.8.
Dk Marco amesema makadirio ya maambukizi ya UKIMWI kwa kila halmashauri hadi kufikia Desemba 2025 kwa halmashauri ya Mji Ifakara imeongoza kuwa na asilimia tano na Manispaa ya Morogoro asilimia 4.4.
Amesema Halmashauri ya wilaya ya Gairo ina maambukizi asilimia 1.5, Kilosa asilimia 3.2 , Malinyi asilimia 2, Mlimba asilimia 3.3, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro asilimia 2.6 na Mvomero asilimia 2.1
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dk Adam Mrisho amesema kwa sasa maambukizi yamejikita kwenye watu wenye umri kuanzia miaka 15, 24 hadi 29 .
Dk Mrisho amesema watu hao wanapatikana maeneo mbalimbali, hivyo mkakati umewekwa kutolewa elimu kwa wanafunzi vyuoni , eneo la madini, uvuvi na njia za masafa marefu.