Wafanyabiashara wahimizwa kuondoa taka

Habari Leo
Published: Jan 26, 2026 09:32:22 EAT   |  Business

WAFANYABIASHARA katika masoko yaliyopo jijini Dodoma wamehimizwa kutosubiri kusimamiwa na viongozi katika uondoaji wa takataka kwenye maeneo yao. Msimamizi wa soko la Sabasaba eneo la miti mirefu Gaudence Temba amesema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanyika kwa zoezi la usafi wa mazingira unaofanyika kila Jumamosi ya wiki.

The post Wafanyabiashara wahimizwa kuondoa taka first appeared on HabariLeo.

Temba amewataka wafanyabishara kuhakikisha wanajisimamia wenyewe badala ya kusubiri mpaka viongozi wawashurutishe kwa ajili ya kufanya usafi huo wa mazingira kwa kusimamiwa. “Niwaombe wafanyabiashara wenzangu suala la usafi wa mazingira liwe ni ajenda ya kila siku na kila mfanyabiashara, tusisubiri usafi huo kufanyiwa na wengine kwa siku ya Jumamosi, bali tuwe tunawajibika wenyewe kwa maslahi yetu ya kulinda afya ya usafi wa mazingira,” alisema.

Msimamizi huyo amewaomba wananchi kwenye maeneo yao kushirikiana na kampuni na vikundi waliopewa dhamana ya uondoaji wa takataka na usafishaji wa taka ili jiji kuliweka safi kiafya. SOMA: Dodoma kutumia takataka kutengeneza gesi, mbolea

Naye msimamizi wa usafi wa mazingira Kitengo cha Afya cha  JHalmashauri ya Jiji la Dodoma,ohn Lugendo amevitaka vikundi vya uzoaji taka kuhakikisha wanawajibika katika uondoaji wa taka mara kwa mara katika maeneo yao waliyopangiwa ili yawe safi. Amesema bado kuna baadhi ya maeneo ndani ya jiji si safi kutokana na miongoni mwa vikundi na kampuni kutowajibika katika kuzoa taka kwa wakati.

The post Wafanyabiashara wahimizwa kuondoa taka first appeared on HabariLeo.