Vijana watakiwa kuchangamkia fursa elimu nje

ARUSHA: VIJANA wametakiwa kuchangamkia fursa za masomo nje ya nchi ili waweze kujiendeleza zaidi kielimu kupitia vyuo vikuu mbalimbali duniani. Akizungumza katika Maonesho ya Elimu ya Vyuo Vikuu nje ya nchi yaliyofanyika Arusha, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Education Link LTD, Abdulmalik Mollel alisema kazi kubwa wanayoendelea kuifanya ni kuwapa fursa vijana wa kitanzania …
ARUSHA: VIJANA wametakiwa kuchangamkia fursa za masomo nje ya nchi ili waweze kujiendeleza zaidi kielimu kupitia vyuo vikuu mbalimbali duniani.
Akizungumza katika Maonesho ya Elimu ya Vyuo Vikuu nje ya nchi yaliyofanyika Arusha, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Education Link LTD, Abdulmalik Mollel alisema kazi kubwa wanayoendelea kuifanya ni kuwapa fursa vijana wa kitanzania kuzifikia ndoto zao kielimu ambapo wanapata ufahamu juu ya kozi gani wanazotaka kusoma, vigezo vipi vinahitajika katika elimu yake ya vyuo vikuu nje ya nchi.
“Wakati Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan akiendelea kuifungua nchi kwenye uwekezaji wa viwanda ,Teknologia, Nishati,Kilimo, Afya na Elimu ni wakati sasa vijana wanapaswa kujiandaa katika rasilimali watu na pia katika Dira ya Taifa 2050 ambapo vijana tunatarajiwa kuchukua fursa ambazo zimefunguliwa katika nchi hii ili tuweze kuhakikisha uchumi wa nchi unakua na ushindani katika bara la Afrika na hata kwa nchi zinzotuzunguka ,”amesema Mollel.
Ameeleza kuwap Global Education link,itaendelea kuunga mkono jitihata za serikali katika kuandaa rasilimali watu hivyo wazazi,wanafunzi,wadau wa vyuo ,shule waelewe uwepo wao katika maonyesho hayo hawatajutia maan awatajionea wenyewe namna fursa hizi zinzvyotolewa na kuwa gharama za masomo zinatolewaa kwa ufadhili wa bure na pia kwa punguzo kulingana na aina ya elimu anayoisomea.
Kampuni hiyo inajihusisha na kutoa fursa za Elimu ya juu nje ya nchi ikifanya kazi kwa mwaka wa 18 sasa itaendelea na kuandaa maonyesho hayo katika mikoa ya Shinyanga ,Mwanza,Dodoma ambapo tayari imefanyika katika Mkoa wa Dar es Salaam na Zanzibar na Arusha.
Mmoja wa Wanafunzi ambaye tayari amepata fursa hiyo kusoma nje ya nchi Danieli kaaya ambaye ni mwanafunzi mtarajiwa wa shahada ya uzamili ameishukuru kampuni hiyo kwani imemuwezesha yeye kufahamu na kuweza kupata nafasi ya kwenda kusoma nchini India itawasaidia kutimiza ndoto zao kielimu.