Ushindi kwa serikali Mahakama ya Rufaa ikiunga ushuru wa nyumba
Mpango wa Rais William Ruto wa nyumba za bei nafuu umepata nguvu kubwa baada ya Mahakama ya Rufaa kuidhinisha sheria ya makazi nafuu na ushuru wa nyumba, huku ikitupilia mbali kesi 42 zilizopinga sheria hiyo.
Katika uamuzi wake, jopo la majaji watano lilisema Sheria ya Makazi Nafuu ilitungwa ili kutekeleza haki ya kila Mkenya kupata makazi bora na ya kutosha kama ilivyo katika Katiba.
Mahakama ilikataa hoja za waliowasilisha kesi wakitaka sheria hiyo itangazwe kuwa batili na serikali iamriwe kurejesha mabilioni ya pesa ilizokusanywa kupitia ushuru huo kutoka kwa waajiri na wafanyakazi.
Kwa mujibu wa sheria hiyo, mwajiri na mfanyakazi huchangia kila mmoja asilimia 1.5 ya mshahara wa mfanyakazi kila mwezi kwa Hazina ya Makazi Nafuu.
Waliopinga sheria hiyo, akiwemo daktari wa upasuaji kutoka Nakuru, Magare Gikenyi, walidai ushuru huo unawalazimisha Wakenya kugharamia nyumba ambazo huenda wasinufaike nazo kamwe.
Pia walidai kuwa jukumu la makazi ni la serikali za kaunti na kwamba serikali kuu ilikiuka Katiba kwa kulitwaa.
Hata hivyo, Mahakama ya Rufaa ilisema makazi ni jukumu kati ya serikali ya kitaifa na zile za kaunti, hivyo sheria hiyo haikiuki mfumo wa ugatuzi.
Majaji waliongeza kuwa ushuru huo hauwezi kutajwa kama ubaguzi au unyakuzi haramu wa mali kwa kuwa serikali ina mamlaka ya kuweka kodi ili kutekeleza majukumu yake ya kikatiba.
Hata hivyo, mahakama ilionya kuwa mpango huo unapaswa kuhakikisha pia unawanufaisha Wakenya maskini zaidi na usitumike kuwanufaisha washirika wa kisiasa au watu wenye ushawishi pekee.
Uamuzi huo unaimarisha moja ya miradi mikuu ya Rais Ruto inayolenga kuongeza upatikanaji wa nyumba nafuu nchini.