Usafirishaji waingiza Dola milioni 2.7, mwaka 2025

Habari Leo
Published: Sep 22, 2026 15:08:26 EAT   |  News

ARUSHA; SEKTA ya usafirishaji nchini imezalisha Dola za Marekani bilioni 2.7 mwaka 2025, sawa na asilimia 15.6 ya mauzo ya nje ya Tanzania, huku thamani hiyo ikiongezeka kutoka takribani dola bilioni 2.2 mwaka 2024 Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, ametoa takwimu hizo leo jijini Arusha alipomwakilisha Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, katika Mkutano …

ARUSHA; SEKTA ya usafirishaji nchini imezalisha Dola za Marekani bilioni 2.7 mwaka 2025, sawa na asilimia 15.6 ya mauzo ya nje ya Tanzania, huku thamani hiyo ikiongezeka kutoka takribani dola bilioni 2.2 mwaka 2024

Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, ametoa takwimu hizo leo jijini Arusha alipomwakilisha Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, katika Mkutano wa Nane wa Afrika wa Usimamizi wa Uendeshaji na Mnyororo wa Ugavi (ACOSCM 2026), unaofanyika kwa siku mbili.

Amesema takwimu hizo zinaonesha kuwa usafirishaji si sekta inayosaidia uchumi pekee, bali ni mhimili muhimu wa uchumi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla, kwa kuwa unaunganisha wazalishaji na masoko, kuwezesha biashara na kuchochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi.

Kihenzile amesema Serikali imeendelea kuwekeza katika miundombinu ya usafirishaji, ikiwemo reli, bandari, usafiri wa majini na anga, hatua inayolenga kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa watu na mizigo na kuimarisha ushindani wa uchumi wa Tanzania.

“Tunapojiandaa kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Serikali imejikita katika kuimarisha usafirishaji, usafiri wa anga na mabadiliko ya kiuchumi yanayotokana na sekta ya usafirishaji,”

Kwa upande wake, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Hawa Tundui, aliwataka watafiti Barani Afrika kuhakikisha tafiti zinazofanywa katika vyuo vikuu zinatafsirika kuwa suluhisho la changamoto halisi zinazokabili biashara, Serikali na jamii, badala ya kubaki katika machapisho ya kitaaluma.

Amesema vyuo vikuu vinapaswa kuendelea kutathmini kile wanachofundisha, namna wanavyofundisha na teknolojia wanazotumia ili kuhakikisha wahitimu wanakuwa na ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko la ajira linalobadilika.