Tanesco yashika nafasi ya pili usimamizi bora wa fedha

Habari Leo
Published: Sep 30, 2026 17:56:59 EAT   |  News

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limepata nafasi ya pili kati ya Mashirika ya Umma ya Huduma na Biashara 306, kwa utendaji bora katika usimamizi wa fedha (Best Financial Management Performance – Commercial Entities). Tuzo hiyo imekabidhiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, Septemba 30, 2026, jijini Arusha, katika kikao …

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limepata nafasi ya pili kati ya Mashirika ya Umma ya Huduma na Biashara 306, kwa utendaji bora katika usimamizi wa fedha (Best Financial Management Performance – Commercial Entities).

Tuzo hiyo imekabidhiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, Septemba 30, 2026, jijini Arusha, katika kikao cha Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi za Umma (CEOs Forum).

Katika utambuzi huo, TANESCO imetambuliwa kwa utendaji wake katika usimamizi wa fedha na rasilimali za Shirika, ikiwemo jitihada za kuhakikisha rasilimali zinatumika kwa ufanisi na kwa kuzingatia uwajibikaji.

Tuzo hiyo imepokelewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO, Plasduce Mbossa, ambaye amesema utambuzi huo ni heshima na pongezi kwa jitihada zinazofanywa na Shirika katika kusimamia fedha na rasilimali zake.

Tuzo hiyo ni sehemu ya utambuzi wa taasisi za umma zinazofanya vizuri katika usimamizi wa fedha, ikiwemo udhibiti wa matumizi, ukusanyaji wa mapato, usimamizi wa rasilimali na kuimarisha uwajibikaji wa kifedha.