Takukuru Mtwara yafanikisha malipo ya Sh milioni 87.3

Habari Leo
Published: May 20, 2026 20:44:02 EAT   |  General

MTWARA: TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Mtwara imefanikisha malipo ya Sh milioni 87.3 za serikali katika sekta binafsi na umma. Yamejiri hayo leo Mei 20, 2026 na Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mtwara Mwanakombo Rajabu alipotoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari juu ya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za …

The post Takukuru Mtwara yafanikisha malipo ya Sh milioni 87.3 first appeared on HabariLeo.

MTWARA: TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Mtwara imefanikisha malipo ya Sh milioni 87.3 za serikali katika sekta binafsi na umma.

Yamejiri hayo leo Mei 20, 2026 na Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mtwara Mwanakombo Rajabu alipotoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari juu ya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha miezi mitatu Januari hadi Machi mwaka huu.

Amesema miongoni mwa fedha hizo zilizofanikishwa katika malipo hayo ikiwemo Sh milioni 34,4 zilizotokana na kutolipwa kwa wakulima 35 wa zao la korosho katika msimu wa mauzo mwaka 2025/2026.

Malipo ya wakulima hao ni kutoka vyama vya msingi (AMCOS) za Namahonga, Langana, kuchele, chimbuko, madaba zilizopo katika Halmashauri ya ya Wilaya ya Tandahimba mkoani humo.

Mbali na hilo wamefanya ufuatiliaji wa miradi 32 ya maendeleo yenye thamani ya Sh bilioni 7.8 katika sekta ya barabara, afya, elimu, maji na mingine.

Pis malalamiko 214 yalipokelewa kati ya hayo asilimia 40 yalihusu vitendo vya rushwa na 60 hayakuhusishwa na vitendo vya rushwa.

  • “Takukuru Mkoa wa Mtwara inawahakikishia wananchi utayari wa kushirikiana nao kwenye mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa na tunawasihi wananchi wote kushiriki katika kudhibiti vitendo vya dhidi ya rushwa,” amesema Mwanakombo.

The post Takukuru Mtwara yafanikisha malipo ya Sh milioni 87.3 first appeared on HabariLeo.