Taifa Stars yaanza kwa kishindo CHAN

Habari Leo
Published: Aug 02, 2025 19:17:10 EAT   |  Sports

DAR ES SALAAM; TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars ‘ imeanza vyema michuano ya Kombe la CHAN 2024 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Burkina Faso mchezo uliofanyika leo Agosti 2, 2025 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Mabao ya Taifa Stars yamefungwa na Abdul Suleiman ‘Sopu’ na Mohamed …

DAR ES SALAAM; TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars ‘ imeanza vyema michuano ya Kombe la CHAN 2024 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Burkina Faso mchezo uliofanyika leo Agosti 2, 2025 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Mabao ya Taifa Stars yamefungwa na Abdul Suleiman ‘Sopu’ na Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’. Michuano hiyo inafanyika kwa mara ya kwanza katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.