TAHARIRI: Ajali hizi za helikopta zimezidi sasa, serikali ichukue hatua hara

Taifa Leo
Published: Oct 12, 2026 16:30:18 EAT   |  News

MFULULIZO wa ajali za helikopta nchini unapaswa kuwaamsha usingizini wenye mamlaka husika. Hatua za dharura zinahitajika ili kuzuia maafa zaidi. Kila mwaka, takribani ajali tano za helikopta huripotiwa nchini, hali inayozua maswali mazito kuhusu usalama wa usafiri huu wa angani na utekelezaji wa sheria zinazousimamia. Ajali ya hivi karibuni iliyohusisha Katibu wa Wizara ya Mazingira, Dkt Festus Ng’eno, na abiria wengine wanne inapaswa kuwa onyo la mwisho kwa serikali. Ingawa waliokuwa ndani ya ndege hiyo walinusurika, rubani alijeruhiwa vibaya huku helikopta hiyo iliyotua katika uwanja wa Kericho Golf Club ikiharibika pakubwa. Kisa hicho hakifai kutazamwa kama tukio moja pekee. Mwezi Agosti, ajali nyingine ya helikopta iliripotiwa Samburu, miezi michache baada ya Mbunge wa Emurua Dikirr, Yohana Ng’eno, kufariki katika ajali ya helikopta mwezi Februari mwaka huu. Matukio haya yanadhihirisha umuhimu wa kuchunguza kwa kina sababu za ajali hizo na kuhakikisha hatua za kuzuia kurudiwa kwa makosa zinachukuliwa. Kinachotia wasiwasi zaidi ni kwamba uchunguzi umekuwa ukifanywa na ripoti kutolewa zikiwa na mapendekezo ya kuimarisha usalama wa usafiri wa angani. Hata hivyo, ikiwa mapendekezo hayo hayatekelezwi kikamilifu, uchunguzi ukibaki kuwa shughuli ya kuwasahaulisha waathiriwa na Wakenya kwa jumla maafa hayo tu. Serikali inapaswa kueleza hatua zilizochukuliwa kutokana na ripoti hizo na kwa nini ajali zinaendelea kutokea. Ripoti kadhaa zimebaini kuwa baadhi ya helikopta zinazotumiwa nchini ni kuukuu na zinahitaji kuondolewa kwenye huduma au kufanyiwa marekebisho makubwa. Ikiwa hali hii imethibitishwa na ukaguzi wa kitaalamu, hakuna sababu ya kuruhusu ndege hizo kuendelea kubeba abiria huku zikihatarisha maisha yao. Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (KCAA) inapaswa kukagua helikopta zote, kuthibitisha ubora wa matengenezo yake na kusimamisha mara moja zile zisizokidhi viwango vya usalama. Aidha, uchunguzi unapaswa kuangazia mafunzo na uzoefu wa marubani, ratiba za matengenezo, hali ya hewa na mifumo ya usimamizi wa safari. Wamiliki na waendeshaji wa helikopta wanaokiuka kanuni wanapaswa kuwajibishwa bila upendeleo. Matokeo ya uchunguzi na utekelezaji wa mapendekezo yake pia yawekwe wazi kwa umma, bila kuathiri taratibu halali za uchunguzi. Serikali haipaswi kusubiri ajali nyingine imeze maisha ya viongozi au raia wasio na hatia ndipo ichukue hatua. Ni wakati mwafaka wa kutekeleza ripoti hizo kwa dhati. Hatua za sasa zitaamua ikiwa usafiri wa helikopta nchini utakuwa salama au utaendelea kuwa chanzo cha hofu na majonzi