Steve Nyerere achangia mil 3/- msiba mama wa Carina

DAR ES SALAAM: MWIGIZAJI Steven Mengele maarufu ‘Steve Nyerere’ ametembelea msibani kwa Fatma Maruzuku mama wa marehemu Hawa Carina aliyefariki dunia leo. Mama huyo amefariki ikiwa ni mwezi mmoja na siku kadhaa tangu kufariki wa mtoto wake Hawa Hussein ‘Carina’. Steve ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao amechangia Sh milioni 3 …
DAR ES SALAAM: MWIGIZAJI Steven Mengele maarufu ‘Steve Nyerere’ ametembelea msibani kwa Fatma Maruzuku mama wa marehemu Hawa Carina aliyefariki dunia leo.
Mama huyo amefariki ikiwa ni mwezi mmoja na siku kadhaa tangu kufariki wa mtoto wake Hawa Hussein ‘Carina’.
Steve ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao amechangia Sh milioni 3 kwa ajili ya rambirambi.
“Tumeguswa sana mama Carina amekuwa pamoja na sisi tangu Carina anaumwa, kiukwei kifo cha mama kimestua, kwa sababu ndani ya mwezi mmoja ametoka kufa mtoto na sasa mama,” amesema Steve.
Steve amesema wasanii pia wameguswa na ndio sababu ya kufika msibani hapo kutoa pole kwa familia ya marehemu.