Singida Black Stars yamkomalia mido Mghana
UONGOZI wa Singida Black Stars, umeonyesha nia ya kumuhitaji kiungo mshambuliaji wa Gor Mahia ya Kenya, Mghana, Enock Morrison, ambaye hadi sasa hakuna mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya huko alipo, pindi uliopo utakapofikia tamati mwisho wa msimu huu.