Simba ilivyoivua ubingwa Yanga
ZANZIBAR; SIMBA jana iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa fainali ya Kombe la Muungano uliochezwa usiku Uwanja wa New Amaan Complex Unguja. Bao hilo pekee katika mchezo huo lilifungwa kwa mkwaju wa penalti na Selemani Mwalimu baada ya Clatous Chama kuchezewa madhambi. Kufikia hatua ya fainali, Yanga ambayo ilikuwa …
The post Simba ilivyoivua ubingwa Yanga first appeared on HabariLeo.
ZANZIBAR; SIMBA jana iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa fainali ya Kombe la Muungano uliochezwa usiku Uwanja wa New Amaan Complex Unguja.
Bao hilo pekee katika mchezo huo lilifungwa kwa mkwaju wa penalti na Selemani Mwalimu baada ya Clatous Chama kuchezewa madhambi.
Kufikia hatua ya fainali, Yanga ambayo ilikuwa bingwa mtetezi iliifunga Azam mabao 2-1 huku Simba ikiifunga Mlandege ya Zanzibar mabao 3-0 mechi zote zikichezwa Uwanja wa New Amaan Complex.
Miamba hiyo itakutana tena Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam Jumapili wiki hii kwenye mchezo marudiano wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kuifanya mechi ya leo kuwa na msisimko wa kipekee.
Kwenye mechi ya Ligi Kuu msimu huu baina ya timu hizo ambayo pia ilichezwa New Amaan Complex Mach Mosi, wababe hao wa soka la Tanzania walitoka suluhu.
The post Simba ilivyoivua ubingwa Yanga first appeared on HabariLeo.