Siasa: Kindiki sasa akimbilia wazee kutafuta nyota

Taifa Leo
Published: Aug 16, 2026 03:55:36 EAT   |  News

NAIBU Rais Kithure Kindiki anaendelea kutumia wazee kuunganisha eneo la Mlima Kenya ili kuwa na umoja wa kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027.
Wiki jana, alikutana na wazee wa jamii ya Ameru Njuri Ncheke waliompa baraka zao.
Jana, Profesa Kindiki alikutana na maelfu ya wazee kutoka Mlima Kenya Mashariki na kuwaomba wazungumze na wenzao wa Mlima Kenya Magharibi kuhusu jinsi eneo hilo lenye wapigakura wengi linavyoweza kuwa na msimamo mmoja.
Akizungumza katika Uwanja wa Nembure, Embu, Profesa Kindiki alisema maeneo hayo mawili yanapaswa kubaki pamoja kwa ajili ya maendeleo.
Hata hivyo, alimshmbulia vikali na mtangulizi wake, Rigathi Gachagua, akimtuhumu kumdhalilisha na kumshambulia kisiasa.
“Nilijaribu kumwambia Gachagua awe na tabia nzuri na apunguze kasi ili Mlima Kenya Mashariki na Magharibi ziishi kwa amani, lakini alikataa. Badala yake aliendelea kunidharau. Hana heshima. Akiendelea kuchafua jina langu, nitamuanika na kushughulika naye,” Kindiki alisema.
Profesa Kindiki pia alimkejeli Gachagua akisema hana hadhi ya kumfundisha siasa.
Profesa Kindiki alisema umoja wa Mlima Kenya Mashariki na Magharibi ni muhimu ikiwa eneo hilo litaendelea kuwa na nafasi katika uongozi wa kitaifa na kunufaika kimaendeleo.
Aliahidi kuhakikisha maeneo hayo yanaungana na kuzungumza kwa sauti moja kuhusu siasa na maendeleo.
Pia alisema maeneo hayo yanapaswa kushirikiana kuhakikisha Rais William Ruto anachaguliwa tena mwaka ujao.
Alimtuhumu Gachagua kwa kugawanya Mlima Kenya kwa maslahi yake ya kisiasa.
“Gachagua anataka Mlima Kenya ugawanyike ili usinufaike na rasilimali za kitaifa. Gachagua ni mtu mbaya na wananchi hawapaswi kumsikiliza,” alisema.
Mkutano huo uliwakutanisha viongozi na wanachama wa mabaraza ya wazee ya Njuri Ncheke kutoka Meru, Nyaangi Ndiriri kutoka Mbeere, Kiama Kia Muembu kutoka Embu na Mwea Council of Elders.
Wazee hao, zaidi ya 30,000 walitaka Profesa Kindiki aheshimiwe kama Naibu Rais na kiongozi wa juu kutoka Mlima Kenya Mashariki.
Walisema wakati umefika kwa Mlima Kenya Magharibi kulipa fadhila kwa kuunga mkono Kindiki bila masharti katika wadhifa wake wa Naibu Rais na katika matarajio yake ya baadaye ya kuwa rais wa kwanza wa Kenya kutoka Mlima Kenya Mashariki.
Wazee hao pia walitangaza Kindiki kuwa msemaji wa kisiasa wa Mlima Kenya, wakisema yeyote anayetaka kuzungumza na wakazi wa eneo hilo kuhusu siasa anapaswa kufanya hivyo kupitia Naibu Rais.
Walitaja miaka ambayo Mlima Kenya Mashariki uliunga mkono viongozi kutoka Magharibi, akiwemo Jomo Kenyatta, Mwai Kibaki na Uhuru Kenyatta, pamoja na manaibu wa rais Joseph Karanja na George Saitoti.
Profesa Kindiki alisema watu wa Mlima Kenya Mashariki wamekuwa wakiunga mkono viongozi kutoka Magharibi bila malalamiko.
Alisema ni jambo la kusikitisha kuona baadhi ya viongozi wakimlipa kwa matusi na kumshambulia kwa maneno, licha ya kuwa yeye ndiye mtu wa kwanza kutoka Mlima Kenya Mashariki kushikilia wadhifa wa pili kwa ukubwa nchini.
Alisema alimpa heshima Gachagua alipokuwa Naibu Rais na hakuwahi kumtukana alipokuwa Waziri wa Usalama wa Ndani.
Kindiki pia aliunga mkono ombi la wazee la mazungumzo rasmi na wenzao kutoka Mlima Kenya Magharibi ili kuunda msimamo mmoja kuhusu mustakabali wa kisiasa, kiuchumi, kitamaduni na kimaendeleo wa eneo hilo.
“Tunaunga mkono ombi la wazee wa Mlima Kenya Mashariki kuzungumza na wazee wa Mlima Kenya Magharibi kuhusu jinsi ya kuunganisha jamii zetu. Tutaheshimu watakachokubaliana,” alisema.
Wazee pia waliomba miradi ya maendeleo ikamilishwe haraka, ikiwemo ujenzi wa barabara ya njia mbili kutoka Makutano kupitia Embu, Chuka, Meru hadi Maua na Daraja la Nithi.