Shughuli zasimama kortini mwanaharakati akipayuka, ‘Hii Kenya tunaongozwa na wezi’!

Taifa Leo
Published: Jan 29, 2026 16:55:45 EAT   |  General

SHUGHULI katika Mahakama ya Milimani zilisimama tisti huku mahabusu na watu wa familia zao wakikimbia kuona kilichokuwa kikiendelea. Watu walifurika katika lango la Hakimu Mwandamizi Carolyne Nyaguthii Mugo huku kila mmoja amevuta shingo. “Kitu gani kinaendelea,” watu waliulizana. “Sijui labda ni mahabusu anajaribu kujinasua,” wakajibizana. Mle ndani ya mahakama - mwanaharakati Julius Kamau alikuwa anang’ang’ana na maafisa wawili wa polisi waliojaribu kumfurusha nje lakini akajikinga. Kamau aliyekuwa amesimama akiegemea ukuta alisema kwa sauti kubwa “Hii Kenya tunaongozwa na wezi. Mbona Wakenya tulichagua wezi. Maisha ni magumu. Mambo ni mabaya. Wananchi amkeni tujitetee.” Baada ya kulipuka hakimu aliacha kusikiza kesi na kumtazama Kamau. Watu waliokuwa mle kortini wameketi walisimama kutoroka huku wanahabari wakimpiga picha za video, simu na kamera. Alipoona kila mtu anamsikiza Kamau alichomoa Bango na kuliinua ili kila mtu kuliona. Wakati huo maafisa wawili wa polisi walimsogelea na kumnyanyua juu. Lakini Kamau alijibanza kwenye kiti cha mahakama na kuvutwa huku akikivuta pia. Polisi walifaulu kumtoa nje kisha akalala kichalichali kwenye sakafu akiendeleza tetezi zake “hata mkinipiga sitaacha kutetea wanyonge.” Polisi hao walimvuta hadi kwenye seli za mahakama akiandamana na wakili Ian Mutiso. Baada ya kukaa mle seli kwa muda aliondoka akiandamana na wakili Ian Mutiso wakatoka. Bw Kamau alikuwa amefika kortini kusimama na David Ooga Mokaya anayeshtakiwa kuchapisha picha ya Rais Ruto katika mtandao wa kijamii akiwa ndani ya jeneza. Mokaya amekana alichapisha habari za uwongo huku akisema “Mimi ni mzalendo siwezi chapisha picha ya rais akiwa ndani ya jeneza.” “Polisi wameniwekelea tu,” Mokaya aliambia mahakama huku akirai, "niachilie nikatafute jinsi ya kujikimu kimaisha nimehitimu chuo kikuu sasa.”