Sherehe, muziki, ghadhabu Eldoret Sikukuu ya Mashujaa
MAELFU ya Wakenya walifurika katika Uwanja wa Kipchoge Keino mjini Eldoret kusherehekea Sikukuu ya Mashujaa, huku muziki, gwaride la kijeshi, nyimbo za kizalendo na mavazi ya rangi za bendera ya taifa yakitawala hafla hiyo.
Sherehe hizo za kitaifa pia ziligubikwa na hasira baada ya uwanja wenye uwezo wa kuchukua watu 15,000 kujaa kabla ya alfajiri, na kuwaacha maelfu ya wananchi nje licha ya kusafiri usiku kucha kuhudhuria.
Kufikia saa tisa usiku, viti vilikuwa vimejaa, huku milango ikifungwa saa kumi na moja alfajiri. Waliokosa nafasi walilalamika kuwa walikuwa wamevumilia baridi kwa saa nyingi wakitarajia kushiriki hafla hiyo ya kihistoria.
Ndani ya uwanja, burudani iliwafurahisha waliofanikiwa kuingia. Kundi la Maroon Commandos, kwaya za kitaifa na wasanii wa eneo hilo walitumbuiza, huku gwaride la kijeshi na maafisa wa vitengo mbalimbali vya usalama likivutia watazamaji. Watoto wa shule na watu wazima walishiriki kuimba nyimbo za kizalendo, huku bendera za Kenya zikipepea. Baadhi ya wananchi walijipamba kwa rangi nyeusi, nyekundu, kijani na nyeupe, huku wengine wakijifunika bendera za taifa.
Lakini nje ya uwanja, hali ilikuwa tofauti kwa sababu polisi walikabiliana na umati uliotaka kuingia, huku baadhi ya wananchi wakilalamikia matumizi ya nguvu na kutengwa katika sherehe zilizokuwa zikifanyika katika eneo lao.
Badala ya kukata tamaa, David Mutua, mkazi wa Kipkaren, aligeuza barabara kuwa ukumbi wa burudani kwa kutumia redio yake kubadilisha hali ya huzuni kuwa shangwe.
Alipocheza nyimbo za kizalendo kama Tushangilie Kenya Taifa Letu Tukufu, Kenya ni Mama Yangu na Naipenda Nchi Yangu, wananchi walianza kuimba, kupiga makofi na kucheza pamoja.
Bw Mutua alisema ingawa hawakuweza kuingia uwanjani, mapenzi yake kwa nchi hayangezuiliwa na kuta za uwanja.
Sherehe hizo pia zilikuwa jukwaa la kuonyesha utamaduni wa jamii za Kalenjin huku wananchi kutoka Uasin Gishu, Nandi na Elgeyo Marakwet wakijitokeza kwa mavazi ya kitamaduni, nyimbo na ujumbe wa umoja.
Hafla hiyo ilikuwa ya kihistoria kwa kuwa kaunti hizo tatu zilikuwa zikishirikiana kuandaa sherehe za kitaifa kwa mara ya kwanza.
Msongamano wa watu ulisababisha foleni barabarani, huku wafanyabiashara wakitumia fursa hiyo kuuza vyakula na bidhaa kwa wageni.