Serikali yazishauri Halmashauri kujenga viwanja vya soka
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amezishauri halmashauri za miji, Manispaa na majiji kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanja vya michezo hasa soka badala ya kuwekeza kwenye kujenga fremu za maduka mara kwa mara.