Serikali yapania makubwa 2026/27 kwenye michezo
SERIKALI imeweka mkakati wa kuibadilisha taswira ya michezo nchini ikilenga kuipandisha Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kutoka nafasi ya 112 katika viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) mwaka 2025 kuingia katika orodha ya timu 50 bora duniani kwa mwaka wa fedha 2026/27.