Saccos Afrika 2026 fursa kwa Watanzania
DODOMA: Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo, amewataka Watanzania kuchangamkia fursa zitakazotokana na Kongamano la 26 la SACCOS Afrika (SACCA Congress – 2026), linalotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 11 hadi 16, 2026. Ameyasema hayo leo, Oktoba 8, 2026, jijini Dodoma, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kongamano hilo litakalowakutanisha …
DODOMA: Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo, amewataka Watanzania kuchangamkia fursa zitakazotokana na Kongamano la 26 la SACCOS Afrika (SACCA Congress – 2026), linalotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 11 hadi 16, 2026.
Ameyasema hayo leo, Oktoba 8, 2026, jijini Dodoma, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kongamano hilo litakalowakutanisha zaidi ya washiriki 1,000 kutoka nchi mbalimbali.
Chongolo amesema kongamano hilo litazinduliwa Oktoba 13, 2026 na Waziri Mkuu Dk Mwigulu Nchemba, likiwa na kaulimbiu inayolenga kujenga uaminifu, kuchochea mabadiliko na kuimarisha mstakabali wa vyama vya kifedha nchini.
Kwa upande wake, Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dk. Benson Ndiege, amesema kongamano hilo litatoa fursa kwa Watanzania kujifunza zaidi kuhusu usimamizi wa Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS), uendelevu wa SACCOS na utawala bora, pamoja na namna ushirika unavyoweza kuwa nyenzo ya kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Aidha, Dk Ndiege amewataka Watanzania kutumia fursa ya kongamano hilo kuitangaza Tanzania kupitia vivutio vya utalii vilivyopo nchini, huku akisisitiza umuhimu wa ushirika katika kuwawezesha wananchi na kukuza maendeleo ya kiuchumi.