Ruto atumia miradi ya maendeleo kujipigia debe kuelekea 2027
RAIS William Ruto anazidi kugeuza maeneo ya ujenzi kuwa majukwaa ya kisiasa, akizunguka nchini kuzindua, kukagua na kukamilisha miradi ambayo imekuwa msingi wa ajenda yake ya maendeleo.
Rais ameweka mabilioni ya fedha katika miradi ya maendeleo akielekea uchaguzi wa 2027, akitegemea barabara, reli, nyumba, masoko, miradi ya maji na huduma za umma kuonyesha rekodi ya serikali yake.
Mkakati huo ulidhihirika wakati wa ziara yake ya siku tano Nyanza iliyokamilika Alhamisi, ambapo alitembelea Kisumu, Siaya, Migori na Homa Bay, akikagua barabara na kuzindua miradi ya maji, afya, elimu na miundombinu.
Ziara hiyo ilijumuisha barabara ya Mamboleo-Miwani-Chemelil-Muhoroni-Kipsitet na miradi ya maji ya Ziwa Victoria huko Kisumu, pamoja na barabara, madaraja, masoko na miradi ya maji Siaya, Migori na Homa Bay.
Badala ya kutegemea miradi mikubwa pekee, Dkt Ruto anawasilisha mtandao wa uwekezaji unaolenga shughuli za kila siku za kiuchumi, zikiwemo barabara bora kwa wakulima na wafanyabiashara, masoko ya biashara ndogo, maji, nyumba za bei nafuu, umeme, hospitali na vyuo vya kiufundi.
Kote nchini, serikali pia inaangazia barabara ya Rironi-Mau Summit, upanuzi wa reli ya SGR hadi Magharibi, nyumba za bei nafuu na mamia ya masoko ya kisasa.
Hata hivyo, wachambuzi wa kisiasa wanasema swali kuu ni iwapo miradi hiyo itasaidia kuongeza mapato ya familia kabla ya Wakenya kupiga kura mwaka 2027.
Dkt Ruto mwenyewe anakiri kuwa gharama ya maisha bado ni changamoto kubwa nchini. Anasema miundombinu inapaswa kuunda ajira, kupunguza gharama ya kufanya biashara na kufungua masoko.
Nyanza kwa mfano, miradi iliyokaguliwa na kuzinduliwa ni pamoja na, Daraja la Dhogoye, Hospitali ya Siaya, uwanja wa michezo na miradi ya maji. Homa Bay ina miradi ya barabara, masoko, maji, nyumba na miundombinu ya baharini, huku Migori ikiwa na miradi kadhaa ya barabara, umeme na masoko.
Miradi mingine mikubwa ni barabara ya Rironi-Mau Summit na upanuzi wa SGR kutoka Naivasha kupitia Narok, Bomet, Kericho na Kisumu hadi Siaya, Kakamega, Busia na Malaba.
Serikali pia inasukuma mpango wa nyumba za bei nafuu, huku Rais akisema inajenga nyumba 300,000, mabweni 180,000 ya wanafunzi na masoko 500 ya kisasa kwa gharama ya Sh93 bilioni.
Kwa mujibu wa Rais, miradi hiyo pia inalenga kuunda ajira na kuweka fedha mifukoni mwa wananchi.
Hata hivyo, wakosoaji wanasema takwimu za ujenzi pekee hazimaanishi moja kwa moja kuwa maisha ya familia yameimarika.
Changamoto nyingine ni muda, kwani baadhi ya miradi mikubwa huenda isikamilike au kutoa manufaa yake yote kabla ya uchaguzi wa 2027.
Kwa hivyo, mtihani wa miradi hiyo hautakuwa idadi ya miradi iliyozinduliwa pekee, bali pia iwapo itakamilika, itafanya kazi na kuleta manufaa yanayoonekana katika maisha ya kila siku ya Wakenya.