Ruto ajitokeza kuchukua hatua mafuriko yakitawala Nairobi tena
Rais William Ruto ameahidi kuwa serikali itaongeza juhudi za kuwasaidia wakazi baada ya Nairobi kukumbwa na wimbi la pili la mafuriko ndani wiki mbili.
Katika taarifa iliyotolewa Jumapili, Machi 15, Rais alisema kuwa kikosi cha pamoja cha taasisi mbalimbali, kinachojumuisha huduma za dharura, idara za usalama, mashirika ya kibinadamu na idara za kiufundi, kitaendelea kuratibu shughuli za uokoaji na kuwahamisha watu walioathiriwa.
Rais Ruto aliongeza kuwa serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na serikali ya kaunti kuhakikisha chakula cha dharura na huduma za matibabu zinawafikia wote walioathiriwa.
“Tunaendelea kufuatilia hali ilivyo kwa karibu, na ninawahimiza Wakenya wote kufuata kwa makini maelekezo yanayotolewa na mamlaka husika, ikiwemo Idara ya Utabiri wa Hewa na polisi,” alisema Ruto.
Alisisitiza kuwa serikali itaendelea kuchukua hatua zote muhimu kulinda maisha ya wananchi, kusaidia jamii zilizoathiriwa na kuhakikisha hakuna Mkenya anayekabiliana na changamoto hiyo peke yake.
Kiongozi wa nchi pia alihakikisha kuwa idara husika zitaendelea kutoa tahadhari na ushauri ili wananchi wawe tayari na wachukue hatua muhimu za usalama.
“Mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu inaendelea kuhatarisha maisha na riziki za wananchi. Mawazo yangu yako pamoja na familia na jamii ambazo tayari zimeathiriwa katika kipindi hiki kigumu,” alisema rais.
Wimbi la pili la mafuriko ya ghafla lililosababishwa na mvua kubwa lilitatiza usafiri katika maeneo kadhaa ya Nairobi usiku wa Jumamosi, Machi 14, baada ya mabomba ya maji kuzidiwa katika vitongoji mbalimbali vya jiji na kufanya barabara kadhaa kutopitika.
Kulingana na Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya, baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko hayo ni pamoja na Parklands,ene la kati kati Nairobi, na barabara ya Ngong karibu na eneo la Ngando, Lower Kabete, Kibera, Kilimani, South B, Kawangware, Lang’ata.
Baadhi ya barabara zilizofungwa kutokana na mafuriko ni pamoja na Nairobi Expressway katika lango la kutokea la Museum Hill, Limuru Road, Bunyala Road Nairobi na Lusaka Road Nairobi, pamoja na mitaa kadhaa ndani ya CBD na Eastleigh.
Shirika hilo ilisema mafuriko hayo yalichochewa zaidi na kujaa kwa mito ya Nairobi na Ngong hali iliyosababisha maji katika maeneo ambayo kwa kawaida hayajulikani kukumbwa na matatizo kama hayo..