RC Sawala: DC Nanyumbu ongeza juhudi utendaji kazi

MTWARA: MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Christopher Magala kuongeza juhudi ya utendaji kazi wa kuwatumikia wananchi katika wilaya hiyo. Rai hiyo imetolewa leo Juni 6, 2025 katika ghafla fupi ya kukabidhi gari kwa mkuu huyo wa Wilaya ya Nanyumbu aina ya Toyota Land cruiser Prado lenye …
MTWARA: MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Christopher Magala kuongeza juhudi ya utendaji kazi wa kuwatumikia wananchi katika wilaya hiyo.
Rai hiyo imetolewa leo Juni 6, 2025 katika ghafla fupi ya kukabidhi gari kwa mkuu huyo wa Wilaya ya Nanyumbu aina ya Toyota Land cruiser Prado lenye thamani ya Sh milioni 252 iliyofanyika katika ofisi ya mkuu huyo wa mkoa.
Amesema Wilaya ya Nanyumbu ni miongoni mwa wilaya ambayo ilikuwa inapata changamoto kubwa ya usafiri katika utekelezaji wa majukumu yao kutoka sehemu moja kwenda nyingine ili kuwafikia wananchi.
RC Sawala ataka bidii kwa wanafunzi Mtwara
“Nikuombe, gari hili likaendelee kuboresha utendaji kazi wako na hasa kuwahudumia wananchi, tunatambua unafanya kazi kubwa sana katika wilaya yako hivyo tunaamini kwa motisha hii kukupatatia chombo kipya kabisa mathubuti utaenda sasa kuwafikia wananchi wetu kwa uharaka zaidi pia mara nyingi zaidi ili kutoa huduma bora kwao,”amesema Sawala.
Naye, mkuu huyo wa Wilaya ya Nanyumbu ameahidi kulitumia gari hilo vizuri kwa maslahi mapana ya taifa kwa kuwaletea maendeleo wananchi wa Wilaya hiyo kwa kufika maeneo ya utawala.
Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Bahati Geuzye amesema Aprili mwaka huu ofisi ya mkuu huyo wa mkoa imefanikiwa kununua gari ambalo amekabidhiwa mkuu huyo wa wilaya katika bajeti ya fedha ya mwaka 2024/2025.
Aidha, wanatarajia kupokea gari lingine hivi karibuni kwa ajili ya Mkuu wa Wilaya ya Masasi ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao.
Pia Juni 2024 walifanikisha kununua magari matatu kwa ajili ya wakuu wa Wilaya za Mtwara, Newala na Tandahimba yenye thamani ya Sh milioni 683 kupitia wakala wa huduma ya ununuzi serikalini (GPSA).
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa amezindua jengo la ofisi za mshauri wa jeshi la akiba lililofanyiwa ukarabati uliyogharimu Sh milioni 49 kutokana na uchakavu wa miundombinu ikiwa ni mwiongoni mwa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kwa bajeti ya mwaka fedha 2024/2025.