Rais Ruto adai ataibuka mshindi uchaguzi ujao

Taifa Leo
Published: Sep 17, 2026 07:55:56 EAT   |  News

RAIS William Ruto amewatahadharisha viongozi wa upinzani dhidi ya kutumiwa na watu aliowataja kuwa “wadhamini wa kisiasa”, akisema serikali jumuishi itashinda uchaguzi wa 2027 kwa kura nyingi zaidi.

Rais Ruto alionekana kumlenga Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, akimlaumu kwa kushindwa kutekeleza mipango ya huduma ya afya kwa wote, nyumba za bei nafuu, maji na elimu alipokuwa madarakani.

Alisema serikali yake imeanza kushughulikia changamoto zilizoachwa na utawala uliopita, kwa usaidizi wa viongozi wa ODM waliojiunga na serikali jumuishi.

“Yule aliyewaajiri alishindwa na UHC, nyumba, maji na elimu. Sasa amekasirika kwa sababu mipango hiyo inaendelea,” alisema.

Rais Ruto pia alikosoa upinzani kwa kile alichodai ni kampeni ya chuki na hujuma.

“Tuliwashinda siku hiyo, na 2027 tutawashinda tena kwa tofauti kubwa zaidi!” alisema.

Huko Migori, Rais Ruto aliahidi Sh124 milioni kukarabati daraja la Mto Migori linalounganisha Suna East na Suna West.

Daraja hilo lilifungwa Februari baada ya sehemu yake kusombwa na mafuriko. Njia hiyo inaunganisha wasafiri kuelekea Sirare na Tanzania.