Raila akumbukwa kwa kupigania mageuzi na demokrasia

Taifa Leo
Published: Oct 08, 2026 16:17:23 EAT   |  News

MAREHEMU Raila Odinga Alhamisi alikumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika kupigania mageuzi ya kisiasa, uhuru wa kidemokrasia na ushirikishaji wa wananchi.

Wasomi, wanahabari na wadau wa siasa waliokutana katika Chuo Kikuu cha Daystar walisema mchango wa Raila kwa demokrasia utakumbukwa na vizazi vijavyo kwa miaka mingi.

Katika kongamano la kumbukumbu la RAO2026 lililodumu kwa siku mbili, washiriki walitafakari safari ya kisiasa ya Raila, kuanzia miaka ya kuzuiliwa gerezani na kupambana akiwa upinzani hadi nafasi yake katika kujenga miungano ya kisiasa, kupigania mageuzi ya katiba na kushiriki katika siasa za kitaifa.

Askofu mteule wa Kanisa la Anglikana Kenya, Dayosisi ya Garissa, Dkt Francis Omondi, alimtaja Raila kama kiongozi aliyefaulu kuunganisha makundi mbalimbali ya kisiasa na mtetezi wa utawala wa kidemokrasia barani Afrika.

“Ni wachache wameacha alama kubwa katika safari ya Kenya kuelekea demokrasia kama Raila Odinga,” alisema Dkt Omondi.

Alieleza kuwa mchango wa Raila haupaswi kupimwa kwa nafasi za uongozi alizoshikilia au uchaguzi aliogombea, bali kwa juhudi zake za kuimarisha demokrasia, utawala wa katiba na ushirikishaji wa kisiasa.

Kwa mujibu wake, kukamatwa, kufungwa gerezani na kuandamwa kisiasa baada ya jaribio la mapinduzi la mwaka 1982 hakukumvunja moyo waka kumfanya akate tamaa, bali kulimfanya kuwa nembo ya mapambano ya kidemokrasia.

Mkurugenzi Mkuu wa Nation Media Group, Geoffrey Odundo, alisema maisha ya kisiasa ya Raila yalijengwa juu ya kujitolea na kujinyima kwa manufaa ya taifa.

“Alivumilia mengi na alipigania demokrasia na uhuru wetu. Tunapaswa kujiuliza tuko tayari kujitolea kiasi gani kwa manufaa ya jamii,” alisema.

Bw Odundo pia alikumbuka uhusiano wa karibu ambao Raila alikuwa nao na wananchi wa kawaida, hasa wakazi wa Kibera, akisema kila alipokabili changamoto za kisiasa au alipokuwa na ujumbe mpya kwa wafuasi wake, angeenda moja kwa moja kwa wananchi.

“Uhusiano wake na wananchi ulikuwa wa kipekee sana,” alisema.

Washiriki wa kongamano pia walitambua mchango wake katika kupigania uhuru wa vyombo vya habari unaofurahiwa nchini leo.

Katika ujumbe wake, Dkt Ida Odinga alisema Raila alichangia kwa kiasi kikubwa safari ya Kenya kuelekea demokrasia na kuhamasisha mamilioni ya watu Afrika na duniani kote.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Daystar, Profesa Laban Ayiro, alisema Raila atasalia kuwa mmoja wa viongozi wenye ushawishi mkubwa katika historia ya demokrasia ya Kenya, huku maisha yake ya kisiasa yakiendelea kuchochea mijadala kuhusu haki, mageuzi ya taasisi na utawala bora.