Rabia: Rais Samia anataka viongozi wawajibikaji

Habari Leo
Published: Sep 23, 2026 17:07:01 EAT   |  News

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Rabia Abdalla Hamid, amesema viongozi wanapaswa kuwajibika kikamilifu katika kuwatumikia wananchi na kutatua changamoto zinazowakabili. Rabia amesema hayo leo, Septemba 23, 2026, wakati akiendelea na ziara ya CCM ya kusikiliza, kuzungumza na kutatua changamoto za wananchi wa makundi …

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Rabia Abdalla Hamid, amesema viongozi wanapaswa kuwajibika kikamilifu katika kuwatumikia wananchi na kutatua changamoto zinazowakabili.

Rabia amesema hayo leo, Septemba 23, 2026, wakati akiendelea na ziara ya CCM ya kusikiliza, kuzungumza na kutatua changamoto za wananchi wa makundi mbalimbali ya kijamii katika Mkoa wa Dodoma.

Katika ziara hiyo, Rabia alikutana na wananchi waliojitokeza na kuwasilisha changamoto, maoni, ushauri na mapendekezo kuhusu masuala mbalimbali yanayowakabili katika maisha yao ya kila siku.

Baada ya wananchi kuwasilisha changamoto zao, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma alijibu hoja hizo na kueleza hatua zinazochukuliwa, huku akiahidi kuendelea kuwatumikia wananchi wa Dodoma.

Rabia alisema Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, anataka viongozi wote wawajibike kikamilifu katika kuwatumikia wananchi na kuhakikisha changamoto zao zinapatiwa ufumbuzi.

Aidha, Rabia aliwapongeza wananchi kwa kujitokeza na kueleza changamoto zinazowakabili, akisisitiza umuhimu wa viongozi kusikiliza na kushughulikia hoja za wananchi.

Mwisho, Rabia alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kazi nzuri ya kuwatumikia wananchi wa mkoa huo, pamoja na kuwa msikivu katika kupokea na kushughulikia changamoto zao.