Pombe haramu yaua watatu Kitengela, wawili mahututi
Huzuni imetanda katika kijiji cha Noonkpoir, Kitengela, Kaunti ya Kajiado, baada ya watu watatu kufariki dunia na wengine wawili kulazwa hospitali wakiwa mahututi kutokana na kile kinachoshukiwa kuwa pombe haramu.
Mnamo Ijumaa asubuhi, Christine na jamaa zake waliomboleza kifo cha mumewe, James Maina Nguru, aliyefariki Jumatatu usiku baada ya kunywa pombe hiyo.
Kwa mujibu wa wakazi, waathiriwa hao walikunywa pombe hiyo katika eneo la Migingo jioni ya Jumatatu kabla ya kufariki nyakati tofauti karibu na makazi yao. Migingo, eneo lililoko Kitengela, limekuwa likihusishwa kwa miaka kadhaa na biashara ya pombe haramu, dawa za kulevya na uhalifu.
Bi Mukeira alisema mumewe, aliyekuwa fundi na baba wa watoto watatu, alirejea nyumbani akiwa katika hali mbaya baada ya kutoka kwenye baa maarufu eneo hilo.
“Alikuwa akilalamika maumivu makali ya tumbo na hakuweza kusimama vizuri. Muda mfupi baadaye alianza kutapika damu na akafariki mbele yetu,” alisema kwa huzuni.
Sasa mjane huyo anasema amelazimika kulea watoto wao peke yake. Familia hiyo imeamua kutofanya uchunguzi wa maiti kutokana na hali ngumu ya kifedha na imani kuwa pombe ndiyo iliyosababisha kifo chake.
Mama yake Nguru, Mary Muthoni, ameitaka serikali kuchukua hatua kali dhidi ya wafanyabiashara wanaosambaza pombe hatari. Alisema mara nyingi alimuonya mwanawe kuhusu madhara ya pombe lakini hakumsikiliza.
Katika eneo hilo hilo, Lynette Sirengo pia anaomboleza kifo cha mumewe, Godfrey Simiyu Kiliswa, aliyefariki baada ya kupatikana akiwa hajitambui karibu na baa inayojulikana kama “Kwa Omosh”. Alifariki siku iliyofuata nyumbani kwake.
Mwanaume mwingine, Elisha Okello, naye alifariki baada ya kurejea nyumbani akiwa amelewa. Mwili wake ulipelekwa katika mochari ya Hospitali ya Kitengela.
Wakati huo huo, ndugu wa mmoja wa manusura amesema mgonjwa amelazwa katika hospitali moja jijini Nairobi akiwa katika hali mahututi, huku viungo vya ndani vikidaiwa kuathiriwa vibaya.
Wakazi wamewalaumu maafisa wa usalama kwa kushindwa kudhibiti uuzaji wa pombe haramu, madai ambayo polisi wamekanusha wakisema wameimarisha msako dhidi ya wauzaji wa vileo haramu na dawa za kulevya. Serikali pia imeagiza operesheni kali kote nchini kukabiliana na biashara hiyo inayozidi kuhatarisha maisha ya wananchi