Omollo atoa wito wa amani Kenya

KENYA: Katibu Mkuu wa Wizara ya Usalama wa Ndani ya Kenya, Raymond Omollo amewataka wananchi wa Kisumu na Wakenya kwa ujumla kudumisha amani katika kipindi hiki cha msiba wa Waziri Mkuu Mstaafu, Raila Odinga. Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuagwa kwa mwili wa Odinga katika Uwanja wa Jomo Kenyatta Mjini Kisumu. Omollo amesema …
The post Omollo atoa wito wa amani Kenya first appeared on HabariLeo.
KENYA: Katibu Mkuu wa Wizara ya Usalama wa Ndani ya Kenya, Raymond Omollo amewataka wananchi wa Kisumu na Wakenya kwa ujumla kudumisha amani katika kipindi hiki cha msiba wa Waziri Mkuu Mstaafu, Raila Odinga.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuagwa kwa mwili wa Odinga katika Uwanja wa Jomo Kenyatta Mjini Kisumu. Omollo amesema amani na utulivu ulioonyeshwa na Wakenya unapaswa kudumishwa hata baada ya tukio hilo.
Aidha, amesema serikali yake itatahakikisha wananchi wengi wanapata fursa ya kuuga mwili wa Odinga.
Zoezi la kuagwa kwa mwili wa mwanasiasa huyo mkongwe nchini linahudhuriwa na maelfu y watu kutoka ndani na nje ya Kenya.
The post Omollo atoa wito wa amani Kenya first appeared on HabariLeo.