Odinga bingwa wa demokrasia -Obama

KENYA: Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama amempongeza kiongozi wa muda mrefu wa upinzani nchini Kenya na Waziri Mkuu wa zamani, Raila Odinga, akimtaja kama “bingwa wa kweli wa demokrasia” ishara thabiti na maridhiano kwa siasa za Afrika. Raila Odinga alifariki dunia Oktoba 15, nchini India ambako alikuwa akipatiwa matibabu. Katika taarifa yake mtandao …
The post Odinga bingwa wa demokrasia -Obama first appeared on HabariLeo.
KENYA: Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama amempongeza kiongozi wa muda mrefu wa upinzani nchini Kenya na Waziri Mkuu wa zamani, Raila Odinga, akimtaja kama “bingwa wa kweli wa demokrasia” ishara thabiti na maridhiano kwa siasa za Afrika.
Raila Odinga alifariki dunia Oktoba 15, nchini India ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Katika taarifa yake mtandao wa X, Obama alisifu harakati za miongo kadhaa za Odinga za kupigania uhuru, haki na utawala bora nchini Kenya.
“Raila Odinga alikuwa mtetezi wa kweli wa demokrasia. Mtoto wa uhuru, alivumilia miongo mingi ya mapambano na kujitolea kwa ajili ya kazi pana ya uhuru na kujitawala nchini Kenya,” Obama alisema.
Mwili wa Odinga utazikwa kesho Oktoba 19, 2025, katika shamba lake la Opoda, Kaunti ya Siaya.
The post Odinga bingwa wa demokrasia -Obama first appeared on HabariLeo.