OCS ashambuliwa na mshukiwa wa uhalifu

Taifa Leo
Published: Oct 14, 2026 18:24:53 EAT   |  News

AFISA Mkuu Msimamizi wa kituo cha polisi (OCS) cha Lamu Central anauguza majeraha aliyopata kwenye makabiliano na  mshukiwa wa uhalifu. Kamanda wa Polisi wa Lamu, Bw Shadrack Ruto, alisema OCS Hassan Noor alikuwa akiongoza kundi la maafisa sita Jumanne mchana kumkabili na kumkamata mshukiwa Ahmed Yusuf Bwanamadi aliyeripotiwa kubeba silaha hatari (panga) huku akihangaisha umma. Licha ya polisi kumwamuru kuweka silaha chini na kujisalimisha mbele yao, mshukiwa alikataa na akamsongea OCS na kumkata sehemu ya mbele ya kichwa. Ni hali iliyowalazimu polisi wengine kutumia bunduki zao ambapo walimpiga risasi mbili za mguu wa kushoto na kumlemaza. Mshukiwa kwa sasa amelazwa kwenye hospitali kuu ya rufaa ya King Fahd kwa matibabu, naye OCS pia anapokea matibabu kwenye hospitali ambayo haikutajwa. Bw Ruto alionya vikali raia wanaoendeleza uvamizi wa mara kwa mara na kuumiza polisi kukoma kwani hatua hiyo ni kinyume cha sheria. Alisema maafisa wake hawatamvumilia yeyote anayewajia kwa lengo la kuwadhuru, akisema wako tayari kutumia bunduki kuyaokoa maisha yao.  