NMG yazindua wiki ya huduma kwa wateja
NATION Media Group (NMG) jana ilizindua maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja katika jumba la Nation Centre, Nairobi, ikisisitiza kujitolea kwake kutoa huduma bora, uandishi huru wa habari na kuboresha huduma zake za kidijitali.
Akizungumza na wafanyakazi na wasimamizi, Mkurugenzi Mkuu na Afisa Mkuu Mtendaji wa NMG Geoffrey Odundo aliwataka wafanyakazi kuwa mabalozi wa kampuni huku wakizingatia viwango vya juu vya huduma na uwajibikaji.
Alisema NMG inalenga kuhudumia wasomaji na watazamaji wake kwa kuwasikiliza na kujibu mahitaji yao.
Maadhimisho ya mwaka huu yanaongozwa na kaulimbiu “The Extra Mile”, huku kampuni ikisisitiza mabadiliko yake kuwa shirika linalotanguliza huduma za kidijitali.