Nairobi yatahadharisha shule kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa matumbwitumbwi

Taifa Leo
Published: Oct 13, 2026 16:21:33 EAT   |  News

SERIKALI ya Kaunti ya Nairobi imetoa tahadhari kuhusu uwezekano wa mlipuko wa ugonjwa wa matumbwitumbwi katika shule, huku wazazi wakishauriwa kuwaweka nyumbani watoto wanaoonyesha dalili za ugonjwa huo hadi watakapopona kabisa.

Kulingana na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Amerika (CDC), dalili za kawaida za ugonjwa huu ni pamoja na kuvimba kwa taya kunakosababisha maumivu, homa, uchovu, kupoteza hamu ya kula na maumivu ya kichwa.

Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema matumbwitumbwi ni ugonjwa wa ghafla unaowaathiri zaidi watoto na vijana, na husababishwa na virusi.

WHO inaeleza kuwa ugonjwa huo kwa kawaida huwa mwepesi na unaweza kupona wenyewe baada ya muda.

Tofauti na magonjwa mengi ya kuambukiza, binadamu ndio viumbe pekee wanaojulikana kuwa wenyeji wa virusi hivyo. Ugonjwa huenea kupitia kugusana moja kwa moja na mtu aliyeambukizwa au kwa matone ya majimaji yanayotoka kwenye mfumo wa juu wa upumuaji.

Afisa Mkuu wa Afya ya Umma wa kaunti hiyo, Tom Nyakaba, aliambia Taifa Leo kuwa tayari ofisi yake imetuma tahadhari kwa shule, ikizielekeza kuhusu namna ya kuzuia maambukizi zaidi.

“Tumeshauri shule kuhakikisha watoto walioambukizwa wanakaa nyumbani,” alisema.

Nyakaba alisema hakuna haja ya hofu kwa sasa kwa sababu idadi ya maambukizi bado ni ndogo na wanafunzi walioathirika wanajitenga ili kuzuia kueneza ugonjwa huo.

“Tumekuwa na visa vya matumbwitumbwi kwa muda wa miezi miwili iliyopita, lakini vimekuwa vikitokea hapa na pale. Kufikia sasa tumerekodi takriban visa 11, lakini maambukizi ya hivi karibuni ni matatu pekee, yaliyoripotiwa katika shule moja eneo la Lang’ata,” alisema.