Mwenge wa Uhuru wazindua miradi Kishapu

Habari Leo
Published: Aug 19, 2026 09:28:21 EAT   |  Sports

SHINYANGA: MIRADI mbalimbali ya Maendeleo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga imezinduliwa na  mbio za Mwenge wa uhuru ikiwemo Soko Kuu la Kata ya Maganzo na Zahanati ya kijiji cha Dugushuli kata ya Igaga. Kongozi  wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Wazo Mwang’onda amezindua leo kwa nyakati tofauti huku akieleza ujenzi wa soko hilo umekokana na  …

SHINYANGA: MIRADI mbalimbali ya Maendeleo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga imezinduliwa na  mbio za Mwenge wa uhuru ikiwemo Soko Kuu la Kata ya Maganzo na Zahanati ya kijiji cha Dugushuli kata ya Igaga.

Kongozi  wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Wazo Mwang’onda amezindua leo kwa nyakati tofauti huku akieleza ujenzi wa soko hilo umekokana na  wawekezaji kutoka kampuni ya Mgodi wa Williamson Diamond Ltd wameweza kutoa fedha hizo za huduma kwa jamii (CSR) kwa mujibu wa sheria na taratibu.

Mwang’onda amewashauri  Wananchi kuunda na kujiunga vikundi  vya watu watano ili kuwa na sifa za kukopesheka fedha za asilimia kumi zinazotolewa na halmashauri bila riba ili wakuze biashara zao.

“Serikali imeweka mikakati kuhakikisha wananchi wake wanakuza uchumi  hivyo wananchi mtumie fursa za masoko yanayojengwa  ambayo ni maeneo rasmi ili kuimarisha biashara na kukuza mitaji”alisema Mwang’onda.

Pia Mwang’onda amesema  zahanati hiyo ameifungua na itaanza kufanya kazi imejengwa kwa nguvu za wananchi na serikali imelamilisha ujenzi wake vifaa tiba vipo ikiwemo kitanda cha kujifingulia wajswazito na dawa na miundombinu hii itunzwe vizuri.

Mbunge wa jimbo la Kishapu Lucy Mayenga amesema wananchi wa Kata ya Maganzo wamefurahi kuwa na soko hilo zuri kwani awali walikuwa na soko ambalo miundombinu yake ni chakavu hali iliyokuwa ikiwafanya washindwe kufanya vizuri biashara na bidhaa kuharibika.

“Suala la zahanati kukamilika nalo limeleta faraja kwani wananchi wa kijiji hiki walikuwa wakilazimika kwenda kujifingua umbali wa kilomota 15 hospitali ya Jakaya kikwete iliyopo Kishapu,”amesema Mayenga.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Peter Masindi alisema Mwenge wa Uhuru utakimbizwa kilomita 128.7 ambapo utapitia miradi minane ikiwa miradi mitano itazinduliwa na mmoja utafunguliwa,mmoja utaonwa na mmoja  utawekwa jiwe la msingi.