Mwenge kukagua miradi ya Sh bilioni 2 Mikindani
MTWARA: MIRADI ya maendeleo 7 yenye thamani ya Sh bilioni 2 iliyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani inatarajiwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru 2026. Mwenge huo umepokelewa leo Mei 3, 2026 mkoani Mtwara katika viwanja vya Shule ya Msingi Mpapura kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara ukitokea mkoani Lindi. Akizungumza wakati wa mapokezi ya Mwenge wa …
The post Mwenge kukagua miradi ya Sh bilioni 2 Mikindani first appeared on HabariLeo.
MTWARA: MIRADI ya maendeleo 7 yenye thamani ya Sh bilioni 2 iliyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani inatarajiwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru 2026.
Mwenge huo umepokelewa leo Mei 3, 2026 mkoani Mtwara katika viwanja vya Shule ya Msingi Mpapura kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara ukitokea mkoani Lindi.
Akizungumza wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Abdallah Mwaipaya amesema Mwenge ukiwa katika manispaa hiyo utaweka mawe ya msingi miradi miwili, utaona na kukagua miradi mitatu pamoja na kuzindua miradi miwili.
Miongoni mwa miradi ya maendeleo itakayopitiwa manispaa ikiwemo kikundi cha vijana cha uvuvi cha mikindani fishers, ujenzi wa kisima cha maji mtaa wa namayanga.
Ujenzi wa madarasa mawili shule ya sekondari shangani, ujenzi wa ofisi ya serikali ya mtaa mji mwema, ufunguzi wa barabara ya mtaa-Namayanga -Naliendele ya kilometa 4.3 na mingine huku ukikimbizwa umbali wa kilometa 106.6.
Naye Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Mwango’nda amewaagiza wataalamu wa miradi wa manispaa hiyo kuwa vifaa vya kupimia miradi viwepo kwenye maeneo yote ya miradi ambayo Mwenge utapitia.
“Niwaombe wataalamu wa miradi wa manispaa kuwa vifaa vya kupimia miradi viwepo kwenye maeneo yote ya miradi ambayo Mwenge wa Uhuru utapitia,” amesitiza Wazo.
The post Mwenge kukagua miradi ya Sh bilioni 2 Mikindani first appeared on HabariLeo.