Mwandishi DailyNews Digital ang’ara Tuzo za TMDA
MANYARA; Mwandishi wa habari wa Dailynews Digital, Aveline Kitomary ameibuka mshindi wa jumla wa uandishi wa habari za dawa,vifaatiba na vitendanishi tuzo zilizotilewa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Tuzo hizo zimetolewa wilayani Babati, mkoani Manyara wakati wa kikao kazi cha wahariri na waandishi wa habari wa Kanda ya Kaskazini inayojumuisha Mikoa ya …
MANYARA; Mwandishi wa habari wa Dailynews Digital, Aveline Kitomary ameibuka mshindi wa jumla wa uandishi wa habari za dawa,vifaatiba na vitendanishi tuzo zilizotilewa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA)
Tuzo hizo zimetolewa wilayani Babati, mkoani Manyara wakati wa kikao kazi cha wahariri na waandishi wa habari wa Kanda ya Kaskazini inayojumuisha Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.
Katika hafla hiyo Aveline amechukua pia tuzo nyingine ya uandishi upande wa kundi la magazeti hii ikiwa ni mara ya tatu kutwaa tuzo hizo.
Akizungumza wakati akipokea tuzo hizo Aveline amesema kuwa siri ya mafanikio hayo ni kujituma na kufanya kazi kwa bidii hasa katika kuandika habari za kijamii.
“Katika kipindi cha mwaka mmoja nimeweza kuandika habari na makala za dawa,vifaa tiba na vitendanishi takribani 19 na hii imekuwa inahitaji bidii kwa sababu kuna makala zingine nimefuatilia muda mrefu tu.
Amewashukuru wahariri wake kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa kazi zinafanywa kwa ufanisi na ubora mkubwa.
“Napenda kuwashukuru mabosi zangu na wafanyakazi wenzangu ushirikiano wao umefanya kufanya kazi bora na zenye weledi,” amesema.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa TMDA ,Yona Mwalu amesema jumla ya kazi 26 ziliwasilishwa ambapo ushindani wa kazi ulikuwa mkubwa.
“Tutaendelea kutoa tuzo na kuongeza zawadi kila mwaka tunataka waandishi wa nchi nzima washiriki katika tuzo hizi, hivyo kwa mwaka ujao tunategemea ushindani zaidi.,”amesema.
Amesema tuzo hizo zinavipengele vitano ambavyo ni kundi la televisheni, redio,vyomba vya habari vya mitandaoni na mshindi wa jumla. Kila kundi mshindi amepata fedha taslimu kiasi cha Sh milioni moja na cheti.