Mwanachuo ashtaki Gavana Mutai akitaka Sh200,000 za malezi

Taifa Leo
Published: Sep 19, 2026 05:55:34 EAT   |  News

GAVANA wa Kericho Dkt Eric Mutai ameshtakiwa mahakamani na mwanafunzi wa chuo kikuu akitaka aagize kumlipa Sh200,000 kila mwezi kwa matunzo ya mtoto wa mwaka mmoja anayesema alizaa naye. M.C, mwanafunzi wa mwaka wa nne katika Chuo Kikuu cha Kabianga, amemshutumu gavana huyo kwa kukwepa jukumu lake la mzazi kwa kukataa kutoa mahitaji ya mtoto huyo, ambaye anadai alizaliwa kutokana na uhusiano wao wa kimapenzi mwaka 2024. Bi M.C pia anataka Dkt Mutai ampe nakala ya kitambulisho chake cha kitaifa ili aweze kupata cheti cha kuzaliwa cha mtoto huyo. Katika stakabadhi zilizowasilishwa mahakamani, mwanafunzi huyo anasema yeye na Dkt Mutai walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi mwaka 2024, ambao ulisababisha kuzaliwa kwa mtoto huyo Julai mwaka huo huko Kericho. Anadai amekuwa akilea na kutunza mtoto tangu kuzaliwa kwake na ndiye amekuwa akigharamia mahitaji yake bila msaada wa maana kutoka kwa gavana. Bi M.C anasema hana ajira wala chanzo cha mapato kwa sababu bado ni mwanafunzi na kwa sasa anategemea ndugu zake kumsaidia yeye na mtoto. Anadai kwamba juhudi zake za mara kwa mara za kumshawishi Dkt Mutai achangie mahitaji ya mtoto hazijafua dafu. “Katika matukio kadhaa tangu mtoto azaliwe, mlalamishi amelazimika kuwasiliana na kumsihi mshtakiwa achangie mahitaji ya mtoto, lakini mara kadhaa simu na jumbe zake hupuuzwa,” inasema sehemu ya stakabadhi hizo. Kwa mujibu wa kesi hiyo, hali ilikuwa ngumu hadi Bi M.C akaondoka Kericho, ambako anaishi kwa kawaida, na kwenda kujisitiri nyumbani kwa dada yake huko Nakuru. Anasema dada yake amekuwa akimsaidia kupata mahali pa kuishi, chakula, matibabu na mahitaji mengine ya msingi akiwa na mtoto wake. Mwanafunzi huyo anadai pia kwamba kutokuwa na kitambulisho cha Dkt Mutai kumezuia mtoto kupata cheti cha kuzaliwa. Anasema hali hiyo imeathiri haki ya mtoto kupata uraia wa kutambuliwa nao. Kesi hiyo iliwasilishwa baada ya juhudi za wawili hao kufikia makubaliano kuhusu matunzo ya mtoto kushindikana. Bi M.C anasema baada ya kumtumia gavana barua ya kumtaka awajibike na kumjulisha kuhusu hatua za kisheria alizokuwa akizingatiwa, Dkt Mutai aliwasiliana naye akitaka suala hilo litatuliwe nje ya mahakama. Kwa mujibu wa mwanafunzi huyo, gavana alipendekeza kutoa Sh25,000 kila mwezi kwa matunzo ya mtoto. Hata hivyo, alikataa kiasi hicho akise ma hakitoshelezi mahitaji halisi ya mtoto. Kupitia mawakili wake, Bi M.C baadaye aliandaa makubaliano ya kugawana majukumu ya malezi na kuyawasilisha kwa mawakili wa gavana. Anasema Dkt Mutai aliwasilisha kesi katika mahakama ya hakimu Nakuru akimshutumu kwa kumzuia kumwona mtoto na kutofichua alikokuwa. Bi M.C amekanusha madai hayo. Anasema Dkt Mutai hajawahi kuonyesha nia ya kumwona mtoto tangu azaliwe wala kufanya juhudi za kupata taarifa kuhusu afya yake, alipo au hali yake kwa jumla. Anadai pia kuwa wakati mmoja alimpeleka mtoto katika makazi ya gavana akitarajia kupata msaada wa matunzo, lakini Dkt Mutai alikataa kumwona au kumshika mtoto huyo. Kulingana na madai yake, baadaye alikatazwa kurejea katika makazi hayo. Mwanafunzi huyo sasa anataka mahakama iamue kwamba haki za mtoto zimekiukwa na iamuru Dkt Mutai kulipa Sh200,000 kila mwezi kwa matunzo yake. Pia anataka gavana huyo awajibikie bima kamili ya matibabu ya mtoto. Katika uamuzi wa Septemba 14, mahakama iliagiza Dkt Mutai akabidhiwe karatasi za kesi ili ajibu madai yaliyowasilishwa dhidi yake. Kesi hiyo itatajwa tena Septemba 28.