Mwaka mmoja tangu Raila alipokufa: Maadhimisho yaanza rasmi

Taifa Leo
Published: Sep 30, 2026 17:12:28 EAT   |  News

CHAMA cha Orange Democratic Movement (ODM) kesho kitazindua rasmi shughuli za mwezi mzima za kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha mwanzilishi wake, Raila Amolo Odinga, kupitia hafla ya kuwasha mishumaa kote nchini. Hafla hiyo itaanza saa kumi na mbili jioni huku Wakenya wakihimizwa kuwasha mishumaa popote walipo kwa heshima ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya. Mwenyekiti wa Kitaifa wa ODM, Gladys Wanga, alisema hafla kuu jijini Nairobi itafanyika katika Bustani ya Uhuru kuanzia saa tisa alasiri. Maeneo mengine yatakayoshuhudia shughuli hizo ni Treasury Square mjini Mombasa, Kisumu Central Square na makao makuu ya Kaunti ya Kajiado. Shughuli hizo zinaashiria mwanzo wa kile ODM imeita “Mwezi wa Baba”, mwezi maalum wa kukumbuka maisha, uongozi na mchango wa Raila katika siasa za Kenya. ODM inasema maadhimisho hayo yanalenga kuwapa Wakenya nafasi ya kutafakari maisha ya Raila aliyefariki nchini India Oktoba 15, 2025 akiwa na umri wa miaka 80. Baada ya hafla ya mishumaa, shughuli hizo zitaendelea katika maeneo mbalimbali nchini. Mnamo  Oktoba 9 kutakuwa na mkutano mkubwa wa kumbukumbu Kakamega huku shughuli za kifamilia zikifanyika kati ya Oktoba 10 na 15 kabla ya ibada kuu ya kumbukumbu katika Kang’o Ka Jaramogi, Bondo, siku ya Oktoba 15. Shughuli hizo pia zitafanyika Garissa, Pwani, Kajiado na Turkana kabla ya kuhitimishwa kwa mkutano mkubwa wa kumbukumbu jijini Nairobi Oktoba 31. ODM imesema maadhimisho hayo hayalengi tu kuomboleza kiongozi huyo wa zamani bali pia kukumbuka maadili aliyosimamia. Katika maisha yake ya kisiasa, Raila alijulikana kwa kupigania katiba mpya, demokrasia ya vyama vingi, ugatuzi na ushiriki mpana wa wananchi katika masuala ya utawala. Chama hicho kimewahimiza wafuasi wake kutumia mwezi huo kujitolea upya katika misingi na maono aliyoyaacha Raila huku kikitafakari mustakabali wake wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027.