Muuguzi aliyejaribu kuokoa maisha ya mbunge Ng’eno atuzwa Mashujaa Dei

Taifa Leo
Published: Oct 20, 2026 17:27:25 EAT   |  News

MUUGUZI Jacobeth Jeptoo ni miongoni mwa Wakenya 264 waliotunukiwa tuzo za heshima wakati wa sherehe za 63 za Sikukuu ya Mashujaa katika Uwanja wa Kipchoge Keino, Eldoret. Walituzwa kutokana na mchango wao katika ukombozi, demokrasia, elimu, uhifadhi wa mazingira na maendeleo ya taifa. Bi Jeptoo alitambuliwa kwa ujasiri wake wa kuwasaidia manusura wa ajali ya helikopta iliyoua Mbunge wa Emurua, Dikirr Johana Ng’eno na watu wengine watano katika Kaunti ya Nandi mnamo Februari 2026. Muuguzi huyo alikimbilia eneo la ajali Chepkiep, Kaunti Ndogo ya Mosop, akiwa na glavu na kujaribu kuwasaidia waathiriwa licha ya hatari iliyokuwepo.Alipewa sifa kwa ujasiri, huruma na hatua za haraka za kuokoa maisha. Miongoni mwa mashujaa wengine waliotambuliwa ni Waziri Mkuu wa zamani Raila Amolo Odinga, mwanaharakati wa demokrasia Philomena Mutai Chelagat, mpiganiaji uhuru Pio Gama Pinto, mwanahistoria Prof Bethwell Allan Ogot, mwanasayansi Prof Calestous Juma na aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani John Michuki. Raila alitunukiwa heshima baada ya kifo chake kwa mchango wake katika demokrasia ya vyama vingi, mageuzi ya katiba na haki za kijamii. Alipinga utawala wa chama kimoja na kusaidia kupatikana kwa uhuru wa kisiasa. Pia alishiriki katika mageuzi yaliyochangia kupitishwa kwa Katiba ya 2010 alipokuwa Waziri Mkuu kati ya 2008 na 2013. Mashujaa wa ukombozi waliokumbukwa ni Koitalel Arap Samoei, Mekatilili wa Menza, Dedan Kimathi na Field Marshal Muthoni wa Kirima. Rais William Ruto pia aliwakumbuka Mzee Jomo Kenyatta na waliokuwa pamoja naye katika harakati za kupigania uhuru. Katika sekta ya elimu na utafiti, Profesa Ogot alitambuliwa kwa mchango wake katika historia ya Afrika, huku Profesa Juma akiheshimiwa kwa utafiti wake kuhusu sayansi, teknolojia na maendeleo. Bw Michuki alitambuliwa kwa juhudi zake za kuhifadhi mazingira, huku mwanariadha Kipchoge Keino na wanamichezo wengine wakipongezwa kwa kuiwakilisha Kenya kimataifa na kung’aa katika fani zao. Rais Ruto alisema kuwakumbuka mashujaa hakupaswi kuishia kwenye sherehe, bali Wakenya wanapaswa kulinda uhuru, demokrasia na Katiba waliyojitolea kuipigania. Alisisitiza kuwa wajibu wa kizazi cha sasa ni kujenga taifa lenye usawa na fursa kwa kila mwananchi.  