Mudathir ni mapafu ya chui

Habari Leo
Published: Aug 03, 2025 08:47:20 EAT   |  Entertainment

DAR ES SALAAM: “Sijui kama mnajua ila najua hamjui kuwa madogo wa siku hizi wamekuwa hawakui watapanga sana safu ila kwangu dafu hawafui, mbio ndefu hizi pub haya mapafu ni ya chui,” Huu ni mstari unaopatikana kwenye wimbo wa Sinaga Swaga wa Young Killer ‘Msodoki’ ‘verse’ ya kwanza. Kwa mujibu wa utafiti wa kituo cha …

DAR ES SALAAM: “Sijui kama mnajua ila najua hamjui kuwa madogo wa siku hizi wamekuwa hawakui watapanga sana safu ila kwangu dafu hawafui, mbio ndefu hizi pub haya mapafu ni ya chui,”

Huu ni mstari unaopatikana kwenye wimbo wa Sinaga Swaga wa Young Killer ‘Msodoki’ ‘verse’ ya kwanza.

Kwa mujibu wa utafiti wa kituo cha wanyama San Diego Park California, chui ni mnyama ambaye anaweza kukimbia sio chini ya mita 200 kwa kasi inayofanana akiamua kuwinda.

Hakuna shaka, Mudathir Yahya Abbas ana mapafu ya chui na mbio ndefu, kwa dakika moja Mudathir anaweza kukanyaga ‘zone’ zote tatu za uwanja kwa kasi ileile, hakika watapanga sana safu dafu hawafui kwa Mudathir.

Mudathir jana amecheza maeneo matatu tofauti, ‘defensive third, ‘half back’ na ‘attacking area’ kinachoshangaza hachoki na kwa ufanisi uleule.

Mudathir amecheza 6, 8, 10 kwa mechi ya jana na kuna wakati dakika za mwanzo alikuwa anaingia hadi kwenye boksi kupiga vichwa. Huyu ni hatari.