Mapenzi si kwa mdomo tu, yawe na vitendo

Taifa Leo
Published: Aug 03, 2025 06:55:44 EAT   |  News

WATU wanapenda kupendwa, lakini wengi hawataki kuwekeza kwenye uhusiano. Wanataka furaha ya kimapenzi, lakini hawataki kazi inayokuja nayo.

Lakini ukweli ni huu: mapenzi bila ukaribu wa kweli ni sawa na gari la kifahari bila mafuta. Litaonekana safi, litasifiwa na majirani, lakini halitafika mbali.

Linabaki hapo hapo, halisongi, haliguswi.Wale walio kwenye ndoa au mahusiano ya muda mrefu wanajua kwamba ukaribu wa kweli sio bahati. Unapaliliwa.

Unatengenezwa kwa maneno matamu, vitendo vidogo vyenye uzito, na muda wa pamoja unaotengwa makusudi, asema mtaalamu wa masuala ya mapenzi Dick Muema.

Unafaa kumshika vizuri mtu wako Si lazima uwe na hela za kumpeleka kujivinjari wikendi. 'Anza na vitu rahisi kama kuzungumza. Na hapa sisemi kupeana taarifa kama 'umelipa stima?', 'umesikia mtoto ana homa?' Hapana.

Zungumza kama mtu ambaye anajali roho ya mwingine. Uliza: “Unaendeleaje moyoni?” au hata “Unajisikiaje nikikukumbatia bila sababu yoyote leo?” aeleza.

Wakati mwingine watu wanakosa ukaribu kwa sababu hawasikilizani. Mko pamoja, lakini kila mmoja yuko makini na simu. "Hio ni ndoa ama WiFi hotspot? Tupa simu pembeni, tazama mwenzi wako machoni. Wewe ni wake, haukuolewa au kuoa kifaa,” asema.

Halafu pia, jamaa, usafi si tu wakati wa harusi. Harufu nzuri, asema Muema, nguo safi, hufanya mtu wako apate hamu ya kukukumbatia bila kuitwa. Ukitoka kazini ukinuka jasho na umkaribie mkeo unamkera.

Tumia maji, sabuni, marashi kidogo na ujue mapenzi nayo yanahitaji maandalizi.Ukaribu hauji kwa kusubiri mwisho wa mwezi. Jifunze kutengeneza muda hata kama ni dakika 30. Mkae chini, mpange mambo yenu.Ukitoka kazini usimwite tu kwa ukali 'uko wapi wewe?' kwa sauti ya kuhoji kama polisi.

Kuwa mpole. Mwambie: “Nilikukumbuka mchana mzima,” hata kama ulikuwa na shughuli nyingi.Kulingana na Muema, mapenzi si mdomo tu. Kuna ngozi. Busu sio tu kwenye midomo pekee.

Jaribu mashavu, shingo, mikono. Mwili wote una neva za mapenzi. Sio kila kitu kiishie kwa “wacha twende chumbani.” Acha mapenzi yaanze mapema pale jikoni, sebuleni, chumbani iwe ni bonasi.”Mapenzi pia yanahitaji mazungumzo ya maana. Si “umeshaoga?” au “tulale?” , uliza maswali yanayofungua roho.

Maswali kama “Unapenda nini zaidi kwangu?”, “Ni ndoto gani hujawahi niambia?” Acha penzi liwe la moyoni, si mwili tu.Pia, wacha kelele. Usilalamike kila siku. Ukimwona amepika viazi badala ya wali, usianze kulalamika. Shukuru kwanza, ukosoaji uje baadaye na kwa staha

. Mapenzi hayawezi kukua kwenye mazingira ya fujo. Ni kama mimea, yanahitaji amani na jua kidogo.Watu wanaombea vyeo kazini lakini hawasali kuhusu mahusiano yao.

Hebu jaribu sala moja pamoja kila jioni. Si lazima iwe ndefu, hata kusema 'Mungu tuimarishe' mkiwa mmekumbatiana ni hatua kubwa.Na mwisho kaka au dada, asisitiza Muema, vaa vizuri.

Usivae kama unahangaika na dunia kila siku. Hata nyumbani, jivishe vizuri. Si lazima uvae nguo mpya – vaa kupendeza. Urembo au mvuto si kwa wageni tu.Mapenzi hayajengwi kwa ahadi kubwa au harusi ya kifahari.

Yanajengwa kwa ubunifu, ukaribu wa kweli, mawasiliano safi, na vitendo vya kila siku vinavyoonyesha kuwa mtu wako ni wa thamani si kwa maneno tu, bali kwa vitendo pia.