Maelfu wapata msaada saikolojia siku 100

Habari Leo
Published: Jan 26, 2026 06:58:21 EAT   |  News

SERIKALI imesema imeimarisha huduma za msaada wa saikolojia na unasihi katika siku 100 za uongozi wa kipindi cha pili cha uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita. Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Dorothy Gwajima watu 171,529 wamehudumiwa ikiwa ni hatua za kuimarisha ustawi wa jamii.

The post Maelfu wapata msaada saikolojia siku 100 first appeared on HabariLeo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Dk Gwajima amesema serikali imeimarisha madawati ya huduma za ustawi wa jamii yaliyopo kwenye vituo vya usafirishaji zikiwemo stendi za mabasi na bandari ili kudhibiti usafirishaji haramu wa watoto.

Dk Gwajima amesema  huduma za saikolojia zinatolewa kwa wazee, watoto waliopo kwenye makao ya watoto, wanaoishi katika mazingira magumu, mahabusu, shule za maadilisho na mahakama za watoto, nyumba salama, manusura wa vitendo vya ukatili na waraibu wa dawa za kulevya. SOMA: Adaiwa kuiba mtoto wa mama mwenye matatizo afya ya akili

Amesema hadi kufikia Desemba mwaka jana watoto 2,699 wakike 1,187 na wa kiume 1,512 walikuwa wameokolewa na kuunganishwa na huduma za ustawi wa jamii na familia zao. Pia, Dk Gwajima amesema watu wazima 2,479, wanawake 1,233 na wanaume 1,246 wamepatiwa huduma za ustawi wa jamii katika madawati hayo.

Amesema katika kuimarisha malezi na makuzi ya watoto chini ya miaka nane imekamilisha mfumo wa ufuatiliaji wa malezi na makuzi ya watoto kupitia kadi ya upimaji. Amesema, mfumo huo utasaidia kubaini ulinganifu katika utekelezaji wa afua za afya elimu ya awali, lishe na ulinzi na usalama wa mtoto.

“Mtoto akifika miaka nane ubongo wake unakuwa umekua kwa asilimia 90 tusipomtengeneza vizuri hapa hatutakuwa na mtoto mzuri huko mbele hivyo tunajikita hapa kwa nguvu zaidi,” alisema Dk Gwajima. Amesema serikali imeendesha mijadala kupitia majukwaa ya wanaume kwa lengo la kutambua mchango wao katika ustawi wa jamii katika kukabiliana ukatili wa kijinsia katika suala la malezi na makuzi.

The post Maelfu wapata msaada saikolojia siku 100 first appeared on HabariLeo.