Kumekucha Tamasha la Pasaka 2026

Habari Leo
Published: Jan 10, 2026 16:10:28 EAT   |  Entertainment

DAR ES SALAAM; Wasanii nguli wa nyimbo za Injili kutoka mataifa mbalimbali wanatarajiwa kuungana na waimbaji wa nyimbo hizo hapa nchini kutumbuiza katika Tamasha la Pasaka mwaka huu. Tamasha hilo huandaliwa na kuratibiwa na Kampuni ya Msama Promotions, ambapo kwa msimu huu litafanyika mikoa 20 likianzia Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama …

The post Kumekucha Tamasha la Pasaka 2026 first appeared on HabariLeo.

DAR ES SALAAM; Wasanii nguli wa nyimbo za Injili kutoka mataifa mbalimbali wanatarajiwa kuungana na waimbaji wa nyimbo hizo hapa nchini kutumbuiza katika Tamasha la Pasaka mwaka huu.

Tamasha hilo huandaliwa na kuratibiwa na Kampuni ya Msama Promotions, ambapo kwa msimu huu litafanyika mikoa 20 likianzia Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama amesema tamasha litaanza Aprili 5, 2026 likizunguka mikoa 20 kukiwa na wasanii mbalimbali wa Tanzania na nje ya Tanzania.

The post Kumekucha Tamasha la Pasaka 2026 first appeared on HabariLeo.