Kero ya maji yamkera Mbunge Ngorongoro

Habari Leo
Published: Dec 12, 2025 11:33:07 EAT   |  Travel

MBUNGE wa Jimbo la Ngorongoro mkoani Arusha, Dk Yannick Ndoinyo ameahidi kufuatilia kujua kwa nini mradi wa maji wenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 6 unasuasua kukamilika kwa zaidi ya miaka saba sasa. Ndoinyo amekutana na kilio cha wakazi wa jimbo hilo maeneo ya Yasi, Mdito, Olorien, Magaiduru, Tinaga, Ngarwa, Mgongo na Mageri katika …

The post Kero ya maji yamkera Mbunge Ngorongoro first appeared on HabariLeo.

MBUNGE wa Jimbo la Ngorongoro mkoani Arusha, Dk Yannick Ndoinyo ameahidi kufuatilia kujua kwa nini mradi wa maji wenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 6 unasuasua kukamilika kwa zaidi ya miaka saba sasa.

Ndoinyo amekutana na kilio cha wakazi wa jimbo hilo maeneo ya Yasi, Mdito, Olorien, Magaiduru, Tinaga, Ngarwa, Mgongo na Mageri katika ziara yake ya siku mbili kukagua miradi ya maendeleo na kuambiwa kuwa tayari zaidi ya Sh bilioni 4 zimetumika katika mradi huo.

Ameeleza kusikitishwa na kusuasua kwa mradi huo uliolenga vijiji nane ndani ya Kata ya Samunge wilayani Ngorongoro, lakini wananchi wanaendelea kuteseka na adha ya maji, wakati serikali imeshatoa asilimia 70 ya fedha za mradi huo.

Amemtaka msimamizi wa mradi huo kuhakikisha unakamilika haraka iwezekanavyo na hawezi kukaa kimya kuona wananchi wake wanatesekana na adha ya maji.

Mwananchi  Steven Ndibaya na amesema changamoto hiyo imewalazimu kutembea umbali mrefu, wakipitia maeneo hatarishi kusaka maji jambo linaloathiri usalama, afya  na muda wa uzalishaji.

Naye Meneja wa RUWASA Wilaya ya Ngorongoro,  Mhandidi Gerald  Andrew, amesema mradi huo umefikia asilimia 50 na juhudi zinaendelea kukamilisha sehemu zilizobaki.

 

The post Kero ya maji yamkera Mbunge Ngorongoro first appeared on HabariLeo.