Kenya yashuka nafasi tano katika viwango vya amani ulimwenguni

Taifa Leo
Published: Sep 19, 2026 03:55:38 EAT   |  General

KENYA imeshuka kwa nafasi tano katika viwango vya amani duniani huku ukosefu wa usalama, migogoro ya kikanda na changamoto za kiuchumi zikiendelea kuhatarisha amani nchini. Katika Global Peace Index (GPI) 2026, Kenya imeshuka kutoka nafasi ya 127 mnamo 2025 hadi ya 132. Alama yake pia imedorora kutoka 2.392 hadi 2.447. Kenya imeshikilia nafasi ya 33 kati ya nchi 44 za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, eneo ambalo, kwa mujibu wa Institute for Economics and Peace (IEP), lilishuhudia kuzorota zaidi kwa amani katika kipindi hicho. Ripoti hiyo imeweka Kenya katika mazingira mapana ya kiusalama ya Upembe wa Afrika, ambako migogoro ya Sudan, Ethiopia, Eritrea, Somalia na Sudan Kusini imeanza kuhusishwa zaidi. “Upembe wa Afrika si mkusanyiko wa migogoro tofauti tena,” IEP ilisema, ikiongeza kuwa migogoro hiyo sasa imeunganishwa kupitia njia mbalimbali zinazowezesha kuenea kwa machafuko.  